title : WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA
kiungo : WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA
WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA
Kamanda wa kanda Maalum, Kamishna Simon Sirro amesema, mbali na wahudumu hao wa chumba cha kuhifadhia maiti, mtuhumiwa mwingine ni Ally Mahamud Nyundo (41) ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kujihusisha na biashara hiyo.
“Watuhumiwa walikamatwa kutokana na kuwepo taarifa ya kupokelewa kwa mwili wa raia wa Ghana katika hospitali hiyo, aliyedaiwa kufariki katika nyumba ya kulala wageni kutokana na kumeza dawa za kulevya,” amesema Kamanda Sirro.
Amesema mtu huyo ambaye bado hajafahamika jina lake alifariki dunia Machi 14 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Red Carpet iliyoko Sinza, wilaya ya kinondoni.
Kamanda Sirro amewataja waliokamatwa kuwa ni Omari Rukola (47) na Athuman Mgonja (48) wote wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti na katika mahojiano walikiri kuuchana mwili wa marehemu na kuchukua kete 32 za dawa za kulevya ambapo alimkabidhi Omary Wagile (47) mfanyabiashara ambaye naye aliziuza kwa Nyundo.
Kamanda Sirro amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Hivyo makala WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA
yaani makala yote WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/wahudumu-wa-hospitali-ya-mwananyamala.html
0 Response to "WAHUDUMU WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA MBARONI KWA KUPAKUA DAWA ZA KULEVYA"
Post a Comment