UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA.

UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA.
kiungo : UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA.

soma pia


UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA.


unnamed
NAIBU INSPEKTA JENERALI WA POLISI, ABDULRAHMANI KANIKI, AKITOA HOTUBA YA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KAMATI TENDAJI ZA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI KWA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA, (SARPCCO)  IKIWA NI MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHIRIKISHO HILO UNAOTARAJIWA KUFANYIKA  JUMATANO TAREHE 24/05/2017 MKOANI ARUSHA. PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.
A
BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI ZA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI KWA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA, (SARPCCO) WAKISIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KAMATI HIZO IKIWA NI MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHIRIKISHO HILO UNAOTARAJIWA KUFANYIKA  JUMATANO TAREHE 24/05/2017 MKOANI ARUSHA. PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI


Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.
Mkutano mkuu wa  mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika jumatano Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu. 
Taarifa iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho la Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za shirikisho hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo mkuu.
 
Bulimba alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa  mbalimbali yakiwemo  dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi. 
 
“Vilevile, mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.
 
SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.


Hivyo makala UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA.

yaani makala yote UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/uhalifu-unaovuka-mipaka-kujadiliwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA."

Post a Comment