TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16

TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16
kiungo : TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16

soma pia


TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16

Image result for picha za mpira wa kikapu
Na Nuru Juma & Husna Saidi-Maelezo.
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linajiandaa kushiriki mashindano ya kanda ya Zone 5 Kimataifa kwa watoto chini ya umri wa miaka 16 yatakayofanyika mjini Mombasa nchini Kenya kuanzia tarehe 1-6 Juni mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es salaam , Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Michael Mwita alisema mashindano hayo yatatumika kupata timu  itakayowakilisha kanda ya Zone 5 na baadaye kuwakilisha  bara la Afrika katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo.
Alifafanua kuwa zimeundwa timu kutoka Mikoa mbali mbali ambapo mazoezi rasmi ya mchujo wa wachezaji kupata timu itakayowakilisha Taifa yataanza tarehe 20 mwezi  huu katika viwanja vya JMK sports Complex jijini Dar es Salaam.
“Tumeshathibitisha ushiriki wa timu yetu na vijana wameshaanza mazoezi tangu mwezi Januari na tumeandaa bajeti ya mil.30 ili kuweza kufanikisha mashindano hayo ambayo kwa Tanzania ni mara ya kwanza kushiriki”, alieleza Mwita.
Aliongeza kuwa mshindi atakaepatikana kwa kanda ya Zone 5 atakutana na washindi wengine wa kanda sita kwa upande wa bara la Afrika na kisha kupata timu itakayowakilisha bara la Afrika na kukutana na bara la Amerika, bara  la Ulaya na bara la Amerika ya Kusini ili kumpata mshindi wa Dunia.
Kwa upande wake kocha wa timu hiyo, Bahati Mgunda alisema ameamua kuteua makocha wasaidizi katika Mikoa mbali mbali ili mchezo huo wa kikapu uweze kuenea nchi nzima.
Mgunda alisema wanahitaji kuwalea watoto wa jinsia zote wenye umri kuanzia miaka 11 hadi 14  watakaopenda kujiunga na mchezo huo wa mpira wa kikapu na baadaye kuwaunganisha katika timu kubwa na kuweza kushiriki mashindano ya Kitaifa.

Katika kanda ya Zone 5 nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Sudan, Sudani Kusini, Uganda, Burundi, Rwanda, Misri na Somalia.


Hivyo makala TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16

yaani makala yote TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/tanzania-kushiriki-mashindano-ya-mpira.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 16"

Post a Comment