SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA

SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA
kiungo : SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA

soma pia


SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo kitaifa yatafanyika katika Hospitali ya St. Gasper halmashauri ya Wilaya ya Itigi tarehe 12 Mei, 2017.

Dkt. Nchimbi amesema hayo mara baada ya kukagua eneo la maadhimisho hayo pamoja na kukutana katika kikao kifupi na watendaji wa chama cha wauguzi Tanzania na watendaji wa hospitali ya St Gasper ambapo maadhimiyo hayo yatafanyika.

Amesema ana imani na uhakika kwa maadhimisho hayo yatafanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na maandalizi mazurri yaliyofanyika huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atawakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.

Dkt. Nchimbi amewataka wauguzi kuitumia siku yao kuonyesha jinsi fani ya uuguzi ilivyokuwa ni fani ya upendo, huruma na kujitoa sadaka katika kuhudumia jamii hivyo wauguzi hao  wajitokeze kwa wingi.

Ameongeza kuwa wananchi wote wa mkoa wa Singida na wale wa halmashauri ya Itigi wajitokeze kwa wingi ili waweze kushirki maadhimisho hayo kwa kupata huduma bure na ushauri juu ya masuala ya afya zao.

Kwa upande wake Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Singida Bi Theresia Ntui amesema maadhimisho ya siku ya wauguzi yatatanguliwa na shughuli ya maonyesho ya shughuli za wauguzi.

Amesema maonyesho yatafanyika katika viwanja vya hospitali ya St. Gasper kuanzia tarehe 10 mpaka 11 Mei 2017 ambapo kutakuwa na huduma za bure kwa wananchi ambazo zitahusisha upimaji wa sukari, shinikizo la damu, Virusi vya Ukimwi na mafunzo kwa vitengo juu ya utengenezaji wa uji wa lishe kwa watoto.

Ameongeza kuwa wananchi wote hasa wazazi wote kuhudhuria mafunzo hayo ya bure ambapo wataelekezwa hatua kwa hatua namna ya utengenezaji wa uji bora wa lishe kwa kutumia vyakula asilia ambapo uji huo utawasaidia watoto pamoja na watu wazima kuwa na afya njema.

Bi Theresia Ntui amewasihi wauguzi wote Mkoani Singida na Mikoa ya jirani kuhudhuria maadhimsiho hayo ambapo wauguzi wote watarudia kiapo chao cha uuguzi pia kutakuwa na  maandamano ambapo watakuwa na fursa ya kuonyesha maoni yao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiteta jambo na Makamu wa Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishauri jambo wakati wa kikao kifupi cha maadalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiagana na Makamu wa Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiagana na Mjumbe wa chama cha Wauguzi Tanzania Alphonsina Kaduma mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.


Hivyo makala SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA

yaani makala yote SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/siku-ya-wauguzi-kitaifa-kufanyika-itigi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA"

Post a Comment