title : SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
kiungo : SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Na Sixmund J. Begashe
Serikali ya Uswisi imeamua kuinga mkoni Serikali ya Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuziwezesha program tano kiasi cha Dola za kimarekani 100,000 ambazo ni takribani Shilingi milioni 220/= ili ziweze kutoa elimu kwa njia za burudani ya mapambano dhidi rushwa nchini.
Akizungumza kabla ya kusaini mikataba ya program hizo, Balozi wa Uswisi hapa nchini Mh ARTHUR MATTLI amesema kuwa Tanzania kwa sasa inafanya vizuri zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa ukilinganisha na nchi nyingi barani Afrika hivyo wameona ni vyema ikaungwa mkono katika mapambano haya.
Balozi Mattli ameongeza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika nchi za Afrika mashariki Tanzania inaongoza katika mafanikio yanayotokana na mapambano dhiri ya rushwa hivyo serikali yake imeona nivyema ikaunga mkono jitihada hizi kwa kuziwezeshwa program zitakazo toa elimu juu ya madhara ya rushwa kwa kupitia sanaa ili watanzania waweze kuipokea nakuielewa elimu hiyo kwa urahisi zaidi.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano ya kupokea fedha za kuendesha programa ya Museum Art Explosion, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti pamoja na kuishukuru Serikali ya Uswizi kwa kutambua jitihada za Makumbusho ya Taifa katika kuelimisha jamii juu ya mambo yanayo wahusu, amemwakikishia Balozi huyo kuwa fedha walizo pata zitatumika kama zilivyo kusudiwa na si vinginevyo.
Nae Mkurugenzi wa Elimu kwa Jamii wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Bw EKWABI MUJUNGU ameishukuru Serikali ya Uswizi kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na Taasisi zilizo wezeshwa na Ubalozi huo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudia ya kupambana na rushwa yanafanikiwa.
Taasisi zilizo wezeshwa ni pamoja Makumbusho ya Taifa kupitia Program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION, Tanzania House of Talent (THT), Kijiji Studii Tanzania, Goba Africa LTD na Art in Tanzania.
Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI na kulia ni Mkurugenzi wa Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure wakishuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti akitia sahii makubaliano ya fedha za kuendeshea program ya Museum Art Explosion kwa mapambano dhidi ya rushwa
Kulia ni Mkurugenzi wa Elimuli kwa Jamii wa TAKUKURU Bw Ekwabi Mujungu na Muanzilishi wa THT Bw Ruge Mutahaba wakimsikiliza kwa Makini Balozi wa Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI(ayupo pichani) .
Hivyo makala SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
yaani makala yote SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/serikali-ya-uswisi-ya-ungana-na.html
0 Response to "SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA"
Post a Comment