title : ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO
kiungo : ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO
ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO
Bweni la wavulana Shule ya msingi Giti iliyopo Wilayani Same limeteketea kwa moto baada ya moto kuunguza bweni pamoja na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.
Wanafunzi wote wamenusurika na moto huo, kwani moto uliwaka majira ya saa 2.00 usiku wanafunzi wakiwa katika vipindi vya usiku darasani.Wanafunzi wamepoteza kila kitu na kuhitaji msaada wa haraka ili kurudisha maisha yao katika hali ya kawaida.
Mkuu wa Wilaya ya Same,Mh DC Same Rosemary Senyamule akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Afisa elimu ,walitembelea eneo la tukio na kuona uhitaji wa marakebisho ya haraka kwa jengo linalotegemea kuhamishia wanafunzi hao ili waendelee na masomo.
DC Rosemary amewataka Wataalamu wa zimamoto na wakaguzi wa shule kufanya kaguzi za mara kwa mara katika taasisi zote ili kuchukua tahadhari za matukio kabla hayajatolea.
Naye Mwenyekiti wa Conference kanda ya kaskazini Mch. Ijiko (kanisa la SDA) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo amewaomba wadau kushirikiana nao ili kurudisha bweni hilo katika hali ya kawaida na kuwawezesha wanafunzi kurudishia mazingira bora ya kusomea.
Tukio hilo litokea Julai 29,2018 kata ya Mamba myamba Wilayani Same.
DC Same Rosemary Senyamule (wa tatu kulia) akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Afisa elimu wakiwa katika kikao cha pamoja mara baada kutembelea eneo la tukio na kuona uhitaji wa marakebisho ya haraka kwa jengo linalotegemea kuhamishia wanafunzi hao ili waendelee na masomo.
Muonekano wa Bweni la wavulana Shule ya msingi Giti iliyopo Wilayani Same lilivyotekea kwa moto baada ya moto kuunguza bweni pamoja na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.
Hivyo makala ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO
yaani makala yote ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/zaidi-ya-wanafunzi-90-wanusurika-na-moto.html
0 Response to "ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO"
Post a Comment