Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini
kiungo : Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini

soma pia


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo muhimu unaokutanisha wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi wa kiserikali unalengo la kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo barani Africa kukutana na kujadili mustakhabali wa maendeleo na uwekezaji barani Afrika.
Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu aliwakilisha Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu (The Education Commission) ambapo alikutana na wadau wa elimu na vyombo vya habari kuelezea Mpango wa Kizazi cha Elimu barani Afrika.
Rais Mstaafu pia alipewa heshima ya kuhutubia hafla ya chakula cha jioni kutathmini mafanikio ya mpango wa Kilimo wa Grow Africa ambao chimbuko lake ni Mkutano wa WEF Africa uliofanyika Tanzania Mei, 2010 na Mpango wa Uwekezaji wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT). 
Katika hotuba yake, Rais Mstaafu alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuchochea ushiriki wa Sekta Binafsi na uwekezaji katika Kilimo barani Afrika. Alitoa angalizo kuwa mafanikio ya mapinduzi ya kilimo hayawezi kufanikiwa kwa kuondoa wakulima wadogo bali kuwaongezea tija. Alitoa rai kwa viongozi wa Afrika kuhakikisha kuwa kilimo cha Wakulima wakubwa kinashamirisha na kustawisha kilimo cha wakulima wadogo na kuwa ni vitu vinavyoweza kwenda pamoja.
Akiwa Durban, Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum. 
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. 
  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pembezoni mwa mkutano huo mjini Durban

  Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum.  
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho akiwa na Mkurugenzio wa World Economic Forum kanda ya Afrikakwenye mkutano huo  unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Kabla ya hapo Bi kanza alikuwa mshauri wa Uchumi wa Rais Mstaafu Kikwete wakati wa uongozi wa awamu ya nne.


Hivyo makala Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini

yaani makala yote Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/rais-mstaafu-dkt-jakaya-kikwete-katika.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika Mkutano wa World Economic Forum on Africa mjini Durban Afrika Kusini"

Post a Comment