title : MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA.
kiungo : MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA.
MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA.
Na Tiganya Vincent, RS- Tabora
31 Mei, 2017
Jumla ya shilingi milioni 180 zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi huo kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waindeshaji wa vyombo vya moto.
Takwimu hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.
Alisema makusanyo hayo yametokana tozo kwa madreva wa magari, pikipiki na bajaji na waendesha baiskeli walivunjia Sheria za Usalama barabarani katika kipindi hicho.
Kamanda alitaja baadhi ya makosa ni madereva wa Bodaboda kutovaa kofia ngumu wao na abiria wao , madereva wa magari kuendesha bila kuwa na leseni, mwendokasi, kutozingatia alama za barabara na kupakia abiria zaidi ya uwezo wa chombo cha usafiri.
Kamanda Mtafungwa alitoa wito kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto Mkoani Tabora kuepuka kuvunja Sheria za Usalama Barabarani ili waokoe fedha wanazozipata zitumike kusaidia familia zao katika matumizi mengine ya maendeleo badala kulipa faini.
“Naomba waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ili wasipigwe faini ambazo zinawafanya watoe fedha ambazo zingewesaidia wao na familia katika shughuli mbalimbali” alisema Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora.
Hivyo makala MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA.
yaani makala yote MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/milioni-180-zakusanywa-mwezi-mei.html
0 Response to "MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA."
Post a Comment