‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA

‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA
kiungo : ‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA

soma pia


‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA


index

 Mwambawahabari
 
Mzunguko wa 30 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefungwa leo kwa vigogo, Simba na Yanga kumaliza na pointi sawa, 68 kila moja baada ya mechi 30.
Hiyo inafuatia Simba kuibuka na ushinid wa 2-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Yanga wakichapwa 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa matokeo hayo, Yanga inafanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu kwa wastani wake mzuri wa mabao, ingawa bado kuna tishio la Simba kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) mjini Zurich, Uswisi kudai pointi tatu za chee walizopokonywa baada ya kupewa kimakosa kufuatia kufungwa na Kagera Sugar.


Baada ya kufungwa 2-1 na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka Uwanja wa Kaitaba, Simba walimkatia rufaa beki Mohammed Fakhi na wakapewa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ikawa pointi tatu, kabla ya Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi na Wachezaji kuwapokonya pointi hizo kufatia Kagera Sugar kukata rufaa pia. 

Mjini Mwanza, katika mchezo huo uliochezeshwa na Ludovick Charles wa Tabora aliyesaidiwa na washuika vibendera Makame Mdogo wa Shinyanga na Vincent Mlabu wa Morogoro, bao pekee la Mbao FC limefungwa na Habib Hajji dakika ya 23.

Mjini Dar es Salaam dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika Simba ikiwa inaongoza 2-1 Uwanja wa Taifa, mabao yake yakifungwa na winga Shizza Ramadhani Kichuya na mshambuliaji Ibrahim Hajib Migomba, huku la Mwadui likifungwa na Paul Nonga.

Kichuya alianza kufunga dakika ya 17 kwa mkwaju wa penalti baada yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kipa wa Mwadui, Shaaban Hassan Kado.  

Na kabla Mwadui hawajakaa sawa, Hajib akawatandika bao la pili dakika ya 24 akimalizia pasi ya Juma Luzio Ndanda. Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Nonga akaifungia Mwadui dakika ya 42 akimalizia krosi ya Hassan Kabunda.

Matokeo ya mechi nyingin Kagera Sugar imeifunga Azam 1-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Stand United imeilaza 2-1 Ruvu Shooting Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Prisons imelazimishwa sare ya 0-0 na African Lyon Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Ndanda FC imeshinda 2-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Mtibwa Sugar imeshinda 3-1 dhidi ya Toto Africans Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji imeshinda 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja Maji Maji Songea.

Hiyo inamaanisha, JKT Ruvu, Toto Africans na African Lyon ndizo zinaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu, zikizipisha Mji Njombe, Lipuli ya Iringa na Singida United zilizopanda kutoka Daraja la Kwanza.

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa mashabiki wa Simba wasiwe na presha kuwa rufaa yao tayari imeshafiika FFA na kusema kuwa hawautambui Ubingwa Yanga mpaka maamuzi yatakapotoka naanaamni kuwa Msimu huu ubingwa Utatua Msimbazi


Hivyo makala ‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA

yaani makala yote ‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/kaburu-hatuutambui-ubingwa-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "‘KABURU’ HATUUTAMBUI UBINGWA WA YANGA,MALALAMIKO YETU FIFA NDIO YATAAMUA"

Post a Comment