title : IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL
kiungo : IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL
IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL
Kampuni ya simu ya Mkononi ya itel imemtambulisha Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa Balozi wa kampuni hiyo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Irene amesema amejisikia faraja kuwa balozi na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu.
Amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na kuweza kufanya makubaliano ya kuwa balozi katika kuunganisha itel na watanzania kwa ujumla.
Kwa upande Mkurugenzi wa itel, Coopeer Chan amesema kuwa wanatarajia jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Irene Uwoya katika matukio ya kuonyesha ukarimu kwa baadhi ya makundi kwa utoaji wa misaada.
Amesema kuwa wanamkaribisha balozi mpya itel Tanzania Irene Uwoya kuungana na familia ya kubwa ya itel.
"Sote tunafahamu mchango wa Irene Uwoya kwenye jamii amekuwa akielimisha kupitia filamu zake na kutambua umuhimu wake sisi itel Mobile tutashirikiana naye kikamilifu kuhakikisha jamii inapata kile inachotarajia kukipata kwetu na kwake pia" amesema Chan.
Mkuruegenzi wa itel, Coopeer Chan akisaini makubaliano na Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency jijini Dar es Salaam.
Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akizungumza na waandishi wa habari juu kuwa balozi wa Kampuni ya Simu ya Mkononi leo jijini Dar es Salaam.
Mkuruegenzi wa itel , Coopeer Chan akibadilishana hati ya makubaliano na Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency jijini Dar es Salaam.
Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akiwa katika picha ya pamoja wafanyakazi itel leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL
yaani makala yote IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/irene-uwoya-balozi-mpya-wa-kampuni-ya.html
0 Response to "IRENE UWOYA BALOZI MPYA WA KAMPUNI YA MKONONI YA ITEL"
Post a Comment