WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI

WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI
kiungo : WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI

soma pia


WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI



 Makomandoo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari lenye tani 7 ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa mapambano.
 Askari wa Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.
 Wanafunzi wa halaiki wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
 Askari wa Pikikipi maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri  leo Mjini Dodoma.
....
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.

“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama

Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.

“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana

Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na  Serikali.


Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka  kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za  vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.


Hivyo makala WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI

yaani makala yote WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/watanzania-waaswa-kuwa-wazalendo-na_25.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO NCHINI"

Post a Comment