title : CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI
kiungo : CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI
CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI
LICHA ya kuchangia asilimia 35 katika pato la taifa, bado sekta isiyo rasmi haijapewa uzito unaostahili kwa kutoshiriki ipasavyo kwenye hifadhi za jamii.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa miaka minne utakaotafiti na kuonesha njia sahihi ya Sekta isiyo rasmi kupata huduma za hifadhi za jamii.
“Tumeona tufanye utafiti ili kuona namna sahihi ya kusaidia waliojiajiri kwenye sekta isiyorasmi kwa kuwa ni kundi kubwa linalofanya biashara ndogondogo zinazochangia karibu asilimia 35 kwenye pato la taifa.
“Katika mradi huu tunaziangalia sekta za aina tatu zisizo rasmi kwanza ujenzi, usafirishaji na wajasiriamali ambao ndio kundi kubwa… kama bodaboda vijana wetu wengi wamejiajiri humu lakini hawana taarifa za kutosha kuhusu haki yao ya kuingia kwenye hifadhi za jamii.
“Hawa mama lishe wengi lakini jiulize wangapi wamejisajili na NSSF? Wangapi wanazo kadi za bima ya afya? Hawa madereva wa bodaboda kila leo wanapata ajali wangapi wanazo bima za matibabu?.
“Hao ndio tunaowazungumzia na tumewaalika kwenye warsha hii waje waseme changamoto zao na tutawaambia namna ya kutoka huko ili wafanye kazi zao kwa furaha na amani wajue kwamba mchango wao kwa taifa ni mkubwa,” alisema Dk. Kinyondo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Utawala na Fedha), Prof. Ernest Kihanga, akisoma hotuba yake kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Miaka Minne utakaotafiti na kuonyesha njia sahihi ya sekta isiyo rasmi kupata Huduma za Hifadhi za Jamii.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Lone Riisgaard kutoka Chuo Kikuu cha Roskilde, akitoa mada.
Hivyo makala CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI
yaani makala yote CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/chuo-kikuu-mzumbe-chajadili-sekta-isiyo.html
0 Response to "CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI"
Post a Comment