SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI
kiungo : SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI

soma pia


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI

Wakazi wa Nchi ya Falme za Kiarabu na wasafiri wa kimataifa watajionea maeneo mbalimbali ya vivutio vinavyopatikana Abu Dhabi kwa siku mbili tu. Shirika la Ndege limezindua shindano hilo kwenye Instagram na zawadi zaidi ya 500 zitashindaniwa.

Shirika la Ndege la Etihad limeamua kuwazawadia mamilioni ya wageni wanaosafiri kupitia makao makuu pamoja na wakazi wa nchi ya Falme za Kiarabu kwa kuleta shindano linalofanyika angalau mara moja kwa mwaka na kuwahusisha watu wote kwa siku mbili.

Kampeni hiyo ya 48 Hour Challenge ni sehemu ya shughuli za Etihad katika kupanua wigo wa kuitangaza Abu Dhabi kama sehemu nzuri ya mapumziko kwa wasafiri na watu wanaopenda kuishi katika nchi ya Falme za Kiarabu hasa wanaopenda kutembelea wakati wa likizo fupi. Wakiwa kwenye jiji hilo watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yameandaliwa kupitia programu hiyo.

Kampeni hiyo ya Shirika la Ndege la Etihad itazinduliwa na msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson ambaye atatangaza jinsi watu wanavyoweza kunufaika na ofa hiyo ya saa 48 wakiwa Abu Dhabi.

Baadhi ya video zake zitaonyesha ofa katika maeneo ya vivutio vya Abu Dhabi. Pia, video za kampeni hiyo zitaonekana kupitia mtandao ambapo wateja watashare na wenzao katika mitandao ya kijamii. Pia wataweza kuona kupitia chaneli za kwenye ndege wanaposafiri.

Wilson alisema, “Kwangu mimi nilijua hii inaamanisha kukaa uwanja wa ndege, au kusafiri bure lakini sivyo kampeni hiyo inavyomaanisha.” 

“Mtu atapata fursa ya kusafiri katika ukanda wa jangwa ikiwa ni pamoja na kutembela maeneo ya kuvutia ya kiutamaduni. Abu Dhabi imenifunza kuwa kutembelea maeneo mbalimbali nikiwa safarini ni sehemu mojawapo ya kuburudika. Hii inaweza kuwa ni miongoni mwa njia nzuri za kupumzika na kujiweka katika hali ya kujisikia vyema. Vilevile nimepata muda wa kujionea mambo mengi kwenye nchi hii. Niwapo safarini sitarudia tena kukaa tu uwanjani na kusubiri ndege tu.”

“Abu Dhabi ni sehemu nzuri, yenye joto kiasi na watu wake wenye ukaribu wa hali ya juu. Mji huu una kila kitu kinachohusiana na mapumziko. Kuna sehemu tulivu na maeneo mazuri ya kutembelea. Ni mji unaovutia na kupendeza ambao una vitu vya kipekee unavyoweza kujionea kwa muda mfupi na kwa wakati.”

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Kuzinduliwa kwa programu hii ya Shirika la Ndege la Etihad kutawawezesha watu kutembelea maeneo mbalimbali wakati wakisubiri kusafiri.
Mohammad Al Bulooki, Makamu wa Rais Mtendaji wa Kitengo cha biashara cha Shirika la ndege la Etihad; Mhe. Saif Saeed Ghobash, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Utalii na Utamaduni (TCA) Abu Dhabi, Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege la Etihad wakisheherekea uzinduzi wa ndege shindano la masaa 48 la kuitangaza Abu Dhabi katika Soko la usafiri la Uarabuni.
Msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson akiruka matuta ya jangwa la Abudhabi wakati aliposhiriki shindano lililozinduliwa na Etihad la masaa 48 ili kuitangaza Abudhabi kwa wasafiri wake.




Hivyo makala SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI

yaani makala yote SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/shirika-la-ndege-la-etihad-lazindua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI"

Post a Comment