title : MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO
kiungo : MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO
MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekabidhi hundi ya Tsh Bil 1 kwa vikundi vya wanawake na Vijana ikiwa ni mchango wa asilimi kumi (10%) ya mapato ya Halmashauri Jiji la Arusha.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Vikundi 269 ambavyo kati ya hivyo 162 ni Vikundi vya wanawake na 107 ni vijana amewataka kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuwatoa katika lindi la umasikini.
“Mikopo hii inatolewa ili kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo zilizopelekea mkidhi vigezo vya kupata Fedha; Nimatumaini yangu fedha hizi zitawawezesha kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi huku mkizingatia nidhamu ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na makundi mengine waweze kupata fedha hizo”Alisema Rc Gambo.
Mikopo hiyo inayotolewa kwa mujibu wa Sheria na miongozo inayoelekeza asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri kutolewe kama Mikopo ya riba nafuu kwa vikundi vya wananwake na vijana na kwa jiji la Arusha kiasi kinachotakiwa kutolewa ni Bil 1.2 kwa Mwaka huu wa Fedha hivyo kiasi kilichotolewa ni kwa kipindi cha robo tatu kuanzia Julai 2016 – March 2017.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Mhe. Gambo amekabidhi vitambulisho 3850 kwa Wazee wa kuanzia miaka 60 ambao ni wakazi wa Jiji la Arusha vitakavyowasaidia kutambulika katika Vituo vvya Afya na kupatiwa huduma za Afya bure.
Kukabidhi kwa Vitambulisho hivyo kunafanya jumla ya Idadi ya vitambulishbo vilivyotolewa na Jiji kwa wazee kufikia 5966 na bado zoezi hili linaendelea kuwabaini wazee wote na kuwatengenezea vitambulisho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo(katikati) akiwakabidhi wawakilishi wa Vikundi vya Wanawake na Vijana mfano wa hundi ya Tsh Bil 1 wakati wa Ziara yake Jijini hapa .kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Mhe. Gabriel Daqaro na Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji Athumani Kihamia.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (katikati kulia) akimkabidhi Mzee Zahran Mtweike (Mbele kulia) Kitambulisho cha Wazee.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia(kulia) akiteta Jambo na Naibu Meya wa Jiji Mhe. Viola Likindikoki wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa Jijini hapa.
Diwani pekee wa Cccm katika Jiji la Arusha Mhe. Abdulrasul Tojo (mbele) akifuatilia nkikao cha Mkuu wa Mkoa wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake Jijini hapa.
Hivyo makala MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO
yaani makala yote MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/mikopo-ya-tsh-bil-1-yatolewa-jijini.html
0 Response to "MIKOPO YA TSH. BIL 1 YATOLEWA JIJINI ARUSHA, WAZEE WAPATIWA VITAMBULISHO"
Post a Comment