title : JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
kiungo : JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
Kitambi ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine kufikia hatua ya kunin’ginia.
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
Kwa wanawake seli hizo zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye makalio.
Kwa upande wa wanaume seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.
Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:
i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
ii. Na njia ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k
SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayo sababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.
VYAKULA VINAVYO CHANGIA KULETA KITAMBI
Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na :
i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta (chips) pamoja na pizza.
ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.
iii. Vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyo ongezwa
( added sugar ), kama vile soda na keki.
iv. Vyakula vilivyo tengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate mweupe nakadhalika
v. Pamoja na vinywaji vilivyo tengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali na kadhalika.
Vyakula vilivyo tajwa hapo juu, vikitumiwa bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia kuleta tatizo la kitambi.
vi. Sababu nyingine ni kutofanya mazoezi ya mwili na viungo
( physical exercises ) kwa muda mrefu.
Hivyo makala JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
yaani makala yote JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/je-unayajua-mambo-yanayo-muweka-mtu.html
0 Response to "JE UNAYAJUA MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI"
Post a Comment