title : Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF
kiungo : Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF
Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF





Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
SHIRIKA la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na Benki za Azania,NMB na NBC kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanachama wake watakao ingia kwenye mpango wa Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, lengo likiwa ni kupunguza hali ya umaskini.
NSSF imeanza utekelezaji wa mpango huu baada ya maboresho ya sheria namba 2 ya mwaka 2018 iliyotoa majukumu kwa shirika hilo kuboresha na kushuhulikia sekta isiyo rasmi ambayo inatajwa kuwa kwa muda mrefu imetelekezwa.
Katika kuhakikisha elimu hii ya inawafikia wananchi wengi ,NSSF imeanza kufanya mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya wajasiriamali ili kutoa hamasa na baadae kuwaingiza katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wananchi wote ambao wako kwenye sekta isyo rasmi..
Mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Moshi,Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Kippi Warioba akatumia nafasi hiyo kutoa rai kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya ubadhirifu.
Kwa upande wao washiriki wa Semina hiyo wakiwemo viongozi wa Benki zilizoingia mkataba na NSSF katika kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanachama walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo wajasiliamali wadogowadogo wameelezea matumani yao juu ya mpango huo wa NSSF.
Wanachama ambao watanufaika na mpango huu ni wale watakao toka kwenye vikundi vyenye sifa za mikopo ambayo itasimamiwa na Benki ya Azania zikiwemo Saccos na Amcos zaidi ya 100.
Mwisho.
Hivyo makala Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF
yaani makala yote Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/sekta-isiyo-rasmin-kunufaika-na-mifuko.html
0 Response to "Sekta Isiyo Rasmin Kunufaika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Kutoka NSSF"
Post a Comment