WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI

WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI
kiungo : WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI

soma pia


WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
SERIKALI ya awamu ya tano imehaidi kushughulikia changamoto za wafanyakazi kote nchini na kuwataka wawe na subira wakati Serikali ikiendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuwahimiza wafanyakazi kutekeleza wajibu wao.

Akijibu changamoto za wafanyakazi kupitia risala  iliyosomwa katika siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimata akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo  amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi kupeleka matatizo ya wafanyakazi katika ofisi husika za Serikali ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa mara moja. 

Aidha ameweka wazi kuwa serikali haitamfumbia macho mwajiri  binafsi ambaye atabainika anamnyanyasa mfanyakazi,na iwapo itabainika  amemnyanyasa mfanyakazi kwa namna yoyote  hatua kali itachukuliwa dhidi take.

"Kuna waajiri ambao wananyanyasa wafanyakazi nimesikia wanawatolea maneno machafu ,wanawapiga ,na wengine hata kuwanyima haki zao sasa nasema viongozi wa wafanyakazi naomba  hatua kali zichukuliwe na sio hivyo tu iwapo  mwajiri yeyote ambaye atabainika anawanyayasa wafanyakazi leteni taarifa ili tuwachukulie hatua Kali" alisema kamanta.

Aidha amesema  kuwa wiki mbili zijazo kiwanda cha matairi general trye kitazinduliwa na serikali itaanza mchakato huo na maagizo ya kuvifuatilia viwanda vingine vilivyofungiwa unaendelea hivyo sherehe za mei mosi sio siku za kuleta changamoto bali ziwe ni furaha.

"Tukae pamoja kabla ya sherehe tuzungumze mapema na tusingoje hadi wakati sherehe hizi za wafanyakazi ndio tunaleta changamoto haileti afya kwani sherehe ni furaha na milango ipo wazi kutatua kabla ya sherehe"amesema kimanta

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi Mwenyekiti Wa chama cha walimu mkoa Wa Arusha Lootha Laizer ameiomba serikali kuwachukulia hatua Kali waajiri wote ambao wanawanyanyasa wafanyakazi.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wamekuwa na tabia ya kuwanyanyasa wafanyakazi kwa kwa kuwapiga, kuwatolea lugha za matusi na hata kuwanyima haki zao  taarifa zao zimetakiwa haraka iwezekanavyo ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.

Akisoma  risala mbele ya mgeni rasmi mratibu wa wafanyakazi Mkoa wa Arusha Samweli Maghero kwa niaba ya wafanyakazi wameiomba serikali kupunguza kodi ya mapato kwa wafanyakazi kwakuwa kodi hiyo ni kubwa na mshahara ni mdogo ukilinganisha na hali ya uchumi.

Aidha pia wameiomba serikali kupandisha madaraja (vyeo )kwa wafanyakazi waliokaa kwa kipindi kirefu bila kupandishwa vyeo ,huku wakiomba  serikali iwape ruhusa ya walimu kuhama vituo vyao vya kazi.
 Mratibu wa wafanyakazi Mkoa Wa Arusha Samweli Maghero akisoma Risala kwa niaba ya Wafanyakazi katika kilele cha siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Baadhi ya wafanyakazi wakifatilia hutuba ya mgeni
  Mwenyekiti Wa chama cha waalimu mkoa Wa Arusha, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Arusha Lootha Laize rakiongea katika maadhimisho hayo ambayo ameiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waajiri wanaonyanyasa wafanyakazi.
 Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimata akihutubia wafanyakazi waliojitokeza kusherekea siku hiyo ambapo amewahimiza kufanyakazi kwa bidii na kuwasilisha matatizo yao kwa wakati.



Hivyo makala WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI

yaani makala yote WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/05/waajiri-watakao-wanyanyasa-wafanyakazi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI"

Post a Comment