title : UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU
kiungo : UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU
UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
Ujenzi holela uliojegwa na baadhi ya wananchi wilaya ya Arumeru imeelezwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha mafuriko yaliotokana na maji kutwaama sehemu moja .
Hayo yamebainishwa na Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati
akizungumza na Wananchi Wa Wilaya hiyo waliokumbwa na mafuriko hayo alipofanya
ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi waliokubwa na mafuriko
ambayo yamepelekea kuharibiwa kwa baadhi ya Mali zao.
Alisema kuwa ujenzi holela uliojengwa na baadhi ya wananchi ndio
umesababisha mafuriko hayo ,kwani wananchi baadhi ya wananchi wamejenga
nyumba katika njia asili zakupitishia maji .
Aidha aliwataka wananchi wote waliojenga mabondeni na kuzuia njia asili za
maji kubomoa Mara moja ili kuepusha mazara makubwa ambayo yanaweza kutokea
hapo baadae kama vifo.
"Mimi nathani hii Mara ya pili hili tatizo kutokea na mwaka Jana lilitokea tena
mmekaa tumekubaliana kuvunja kuta zote ambazo zinazuhia maji kupita kwenye
mkondo wake hivyo basi najua kunawatu wataathirika lakini inabidi ili
tuweze kutatua tatizo kubwa linaloweza kutokea apo baadae" alisema Muro
Aliwataka wananchi kufuata sheria za ujenzii wa miipango miji nakuacha kujenga kiholela holela ilikuondokana na adha inayoweza kuutokea.
Kwa upande mmoja ya moja ya mwananchi alieathirika Rose Nassari aliishukuru serikali kwa kuwatembelea na kuwapo pole pamoja na kuwapa elimu ya hasara ya kujenga kwenye mikondo ya maji.
Mafuriko hayo yamekumba katika baadhi ya kaya za vijiji vya nduruma pamoja na shangarai. picha ikionyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiongea na wananchi wa wilaya hiyo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wake waliokubwa na tatizo mafuriko ,ambapo alisema ujenzi hoela ndio chanzo cha mafuriko hayo na kuwataka wananchi waachie njia za asili za maji ili yaweze kupita
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na Wananchi wa wilaya hiyo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wake waliokubwa na tatizo mafuriko ,ambapo alisema ujenzi hoela ndio chanzo cha mafuriko hayo na kuwataka wananchi waachie njia za asili za maji ili yaweze kupita
Picha ikionesha mwananchi mmoja wa kijiji cha Shangarahi akiwa
amebebwa mgongoni tayari kwa kuvushwa daraja mara baada ya daraja hilo kusombwa na maji.
Hivyo makala UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU
yaani makala yote UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/05/ujenzi-holela-chanzo-mafuriko-arumeru.html
0 Response to "UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU"
Post a Comment