Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania

Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania
kiungo : Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania

soma pia


Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania



Mwandishi Phelisters Wegesa Marwa

Nyumbani mbali na Nyumbani Jamhuri ya Watu wa China, nashukuru sana hii yote ni kwa sababu ya urafiki mwema kati ya China na Tanzania naishi kama nyumbani. Mnamo Agosti 2016 nilifunga mizigo yangu na kusafiri angani takriban maili 5,340 kutoka Dar es Salaam, mji wa kibiashara wa Tanzania hadi Beijing nchini China kutafuta maarifa. 
Hapo awali nilikuwa nimeshaenda nje ya nchi Tanzania kwenye vikao, semina, kazi Afrika na hata Ulaya, ambapo nilikaa wiki chache au miezi michache. Lakini China bila shaka ni tofauti na nchi zinazozungumza Kiingereza na Kiswahili na kwa nchi ya China Kichina ni lugha inayotumika zaidi. Watu wengi wana dhana kuwa kuja China zaidi ni kufanya biashara na sio Kusoma: Lakini bado nilisisitiza nitakuja China, nilitaka kueleza uamuzi wangu wa kujifunza nje ya nchi na kwamba kuna mengi zaidi duniani ya kujifunza zaidi ya Marekani na mimi niilitamani kuyajua haya .

Kwa heshima ya kuchaguliwa na Ofisi ya Uchumi na Biashara ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, kwa ufadhili kutoka Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China (MOFCOM) katika Chuo Kikuu cha Beijing ambacho kwa sasa pia ni Taasisi ya Utafiti wa Belt na Road. 

2019 ni mwaka wa kusherehekea miaka 55 ya mahusiano ya kidiplomasia ya China na Tanzania; China na Tanzania wana ndoto ya pamoja. Ndoto ya ushirikiano wa kiuchumi na ushirikiano wa maendeleo ya pamoja, ndoto hii na ushirikiano kati ya China na Tanzania inarudi nyuma ya kumbukumbu ya miaka kadaa iliyopita wakati hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alikutana na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong. 

Historia ya Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), mradi mkubwa zaidi wa msaada wa kigeni nchini Afrika hadi sasa na uwekezaji mwingine unaoungwa mkono na serikali ya Kichina; Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Urafiki, Shamba la mpunga la Mubarali, Mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Kiwanda cha miwa cha Mahonda, Uwanja wa Taifa , Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Maktaba ya Kimataifa ya sanaa ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, bandari ya New Bagamoyo pamoja na mtandao wa reli unaounganishwa na reli nyingine za Tanzania na kadhalika. Historia hii ina maana kubwa sana katika uhusiano kati ya China na Tanzania na hata Afrika kwa ujumla. 
Mwenyekiti wa muda mrefu China, Mao Zedong pamoja na Rais wa kwanza wa Tanzania, J. K. Nyerere, Machi 25, 1974.

China na Tanzania wanaendelea kuimarisha uaminifu wa kisiasa kwa njia ya ziara za mara kwa mara za viongozi wa serikali. Rais wa China Xi Jinping alichagua Tanzania kuwa kituo chake kwanza cha ziara yake ya Afrika mwaka 2013 baada ya kuchukua madaraka na hii inathibitisha umuhimu wa mahusiano ya China na Tanzania. 

Aidha, kumekuwa na ziara nyingi za juu za kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili kwa uzinduzi wa miradi mbalimbali zaidi; ikiwa ni pamoja na Elimu, Miundombinu, Afya, Utalii, Mbinu za Kilimo za Kisasa, Mauzo ya Nje na Uagizaji ambayo umeimarisha uhusiano zaidi na kubadilishana uzoefu. 
Rais wa China Xi Jinping (Kulia) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa FOCAC mjini Beijing, Septemba 6, 2019.

Tanzania imejihusisha kushiriki kikamilifu katika Mpango wa Belt na Road na Septemba iliyopita, Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika (FOCAC) walikubaliana na Rais Xi Jinping kuendelea kuimarisha ushirikiano wenye manufaa kati ya pande zote mbili. China inasaidia juhudi za Tanzania katika kulinda haki na maslahi yake, kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu, na iko tayari kuimarisha na kubadilishana uzoefu wa utawala, maendeleo na mikakati ya kupunguza umaskini. 

China bila shaka ni kinara duniani katika kupunguza umaskini na kuna mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wake. China inachukua jukumu zaidi katika hatua ya kimataifa na Tanzania ina nafasi nzuri ya kuendelea kushirikiana zaidi na nchi nyingine zinazoendelea kujifunza kutoka China na kufanya kazi pamoja kuwekeza katika nguvu zake za viwanda na uvumbuzi. 

Wizara ya Afya na wadau muhimu kutoka Tanzania na China wamekutana mara kwa mara kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Afya kwa njia ya miradi ambayo tayari imeanzishwa. Mfano mkubwa ni Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ndio taasisi ya moyo ya kwanza nchini Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mnamo Oktoba 2015, JKCI imefanikiwa kutibu maelfu ya wagonjwa wa moyo na kufanya upasuaji wa moyo zaidi ya 1,500 kwa gharama nafuu, na hivyo kuleta faida kubwa kwa watanzania. 

Hivi sasa, kuna madaktari watatu wa kichina wanaofanya kazi JKCI, waliobobea katika upasuaji wa moyo na magonjwa ya watoto. Hivi karibuni JKCI imesaini mkataba wa makubaliano na Hospitali ya Fuwai iliyopo nchini China ambayo ni kituo kikubwa kinachoshughulikia matatizo ya moyo na kinachojulikana duniani na kimataifa kwa matibabu sugu ya aina tofauti sumbufu ya moyo. 
China imeonyesha kujitolea kwa kupanua upatikanaji wa huduma za afya, kuanzia na Mfumo wa Matibabu wa Ushirika, upatikanaji wa ubora wa huduma za afya ambayo imekuwa mojawapo ya eneo la msingi la Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China na Wizara ya Afya Tanzania na ni kupitia miradi hii ya pamoja na mafunzo ya wataalam na ushirikiano wa taasisi za afya. 

Zaidi Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu alikutana na Waziri wa Afya wa China Ma Xiaowei na kusema kuwa China itaendelea kupeleka timu za matibabu Tanzania kwa kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika matibabu ya angiocardiopathy, kansa, afya ya umma, pamoja na mafunzo ya madaktari wa kitaaluma na ujanibishaji wa bidhaa za dawa. Ilihitimishwa kwa kusaini mkataba wa ushirika kati ya Hospitali ya Saratani ya Kichina ya Sayansi ya Matibabu ya China na Taasisi ya Saratani Ocean Road Tanzania. 
Waziri wa Afya Mheshimiwa Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na wataalamu wengine wa afya kutoka China na Tanzania wakati wa ziara ya Hospitali ya Kimataifa ya Peking University (PUIH). 

Watanzania wana kila sababu ya kudumisha uhusiano wa China na Tanzania na mustakabali wa mahusiano haya yapo mikononi mwa vijana wote waliopata nafasi ya kuja kujifunza nchini China na kujifunza hata kwa Wachina nyumbani. Ni jukumu la vijana kufanya bora zaidi kwa yale tuliyojifunza, ni funguo katika kukuza maendeleo mapya na mafanikio ya nchi ya Tanzania. Hii itasaidia kuongeza kasi ya mageuzi na mabadiliko yaliyopangwa na Mheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa John Joseph Magufuli. 

China kama mshirika muhimu wa maendeleo na Tanzania, Tanzania inahitaji China katika mkakati wa viwanda ili iweze kufikia lengo la kuwa uchumi wa katikati mwaka 2025 kwa kuzingatia taarifa ya "2019 ni mwaka wa uwekezaji". 

Mustakabali wa kesho unaonekana kuwa mzuri na wenye mafanikio, nikitizama mbele naamini na naona kuwa kuunganisha umuhimu wa ushirikiano wa elimu ya juu, sayansi na teknolojia, utafiti ni suluhisho muhimu kuimarisha uchumi wetu. Nina hakika kwamba msingi wa urafiki uliojengwa na China na Tanzania utafikia kizazi cha baadaye kwa kufanya kazi pamoja ili kujenga jumuiya yenye nguvu zaidi ya baadaye. Siku hiyo itakuja wakati taifa la Kichina litafikia ndoto yake ya upyaji wa kitaifa na Tanzania itafahamu na kuelewa ndoto yake ya umoja na kuendelea kuimarisha! 


Udumu Urafiki wa China na Tanzania! 

Phelisters Wegesa Marwa 

Mtumishi wa Umma anayefanya kazi 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Tanzania na ni mwandishi wa kujitegemea wa makala ya Uchumi, Vijana, Elimu na Ushirikiano wa China na Afrika. 


Hivyo makala Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania

yaani makala yote Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/05/makala-ya-kuadhimisha-ushirikiano-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania"

Post a Comment