Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu

Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu
kiungo : Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu

soma pia


Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu

Dodoma. Benki ya NMB wamekubali kusaidia wakulima wa zao la zabibu mkoani Dodoma,ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali wa kuwainua wakulima.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NMB Albert Jonkergouw katika hafla fupi ya benki hiyo kwa taasisi za serikali, viongozi wa taasisi na wafanyabiashara iliyofanyika katika ukumbi wa new Dodoma hotel.Mkurugenzi huyo alisema nguvu kubwa imeelekezwa kwa wakulima kutokana na sera ya Tanzania ya viwanda lakini akasifu mpango wa serikali kuhamia Dodoma ambao umeungwa mkono na benki hiyo.

Jonkergouw alisema katika kuunga mkono uhamiaji Dodoma, NMB wameshapeleka tawi la benki tembezi katika mji wa kiserikali Mtumba na kwamba mipango ya baadae ni kufanya maboresho makubwa ya huduma za benki katika eneo hilo.

“Tutaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara, mimi niseme kuwa benki hii ni mali yenu mna haki ya kuitumia nasi ni wajibu wetu kuwahudumia,” alisema Mkurugenzi.

Akizungumza katika halfa hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge aliomba uongozi wa NMB kuutazama mkoa wa Dodoma kwa jicho la pekee kutokana na ongezeko la watu kufuatia ujio wa makao makuu.

Dk Mahenge aliomba benki kurahisisha masharti katika upatikanaji wa mikopo ikiwemo kuwapa kipaumbele zaidi wakulima wa zabibu zao linalotajwa kuwa mkombozi kwa wenyeji w amkoa huo.

Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamini Mkapa ya Jijini hapa Dk Alfonce Chandika alisema benki ya NMB ni rafiki kwa makundi yote kutokana na huduma zake kuyagusa makundi yote.

Dk Chandika alisema kwa sasa huduma zinazotolewa na benki hiyo zinapaswa kuwa mfano kwa taasisi zingine jambo litakalotoa tafsiri chanya kwa Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Albert Jonkergouw akiongea na watumishi wa Serikali na wafanyabiashara kwenye chai ya Asubuhi iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma jana. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR. Binilith Mahenge (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Albert Jonkergouw (Kulia) kwenye chai ya Asubuhi iliyo andaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma jana.


Hivyo makala Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu

yaani makala yote Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/05/benki-ya-nmb-yaahidi-kusaidia-wakulima.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu"

Post a Comment