NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO
kiungo : NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

soma pia


NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani
Mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiongea na wanafunzi walijitokeza kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa



NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

NAIBU MEYA wa manispaa ya Iringa amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani.

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mwembetogwa,Lugalo,Tagamenda na Mawelewele naibu meya Joseph Lyata aliwataka wanafunzi hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.

Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo” alisema Lyata

Lyata alisaema kuwa nchi nyingi ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.

“Angalieni nchi kama Somalia tu hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu” alisema Lyata

Lyata aliongeza kwa kusema kuwa uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa wazalendo na nchi yao.

“Lazima tuambizane ukweli kabisa maana sisi kama manispaa tunahakikisha manispaa inaendelea kuongoza kwenye usafi,kuhakikisha wanafunzi mnasoma vizuri bila kuwa na woga na kuhakikisha tunailinda mipaka ya nchi yetu huo ndio uzalendo wa nchi yetu” alisema Lyata

Lyata aliwata wanafunzi kuanza kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.

“Uzalendo pia huanzia pale unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Lyata

Naye mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.

“Wananchi wanasababisha umasikini wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio hupelekea umaskini katika kwa wananchi waliomchagua kiongozi waliyekuwa na imani naye,hivyo kukosea kuchagua kiongozi bora ni kujitafutia matatizo wenyewe” alisema Ngerera

Ngerera aliongeza kwa kuwaambia wanafunzi hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri huo waliona wanafunzi kwa kuwa ndio kipendi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.

“Jamani lazima mjifunze mnapotaka kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza mlikosea wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku mkiwa mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Ngerera


Hivyo makala NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

yaani makala yote NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/naibu-meya-joseph-lyata-awataka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO"

Post a Comment