Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17

Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17
kiungo : Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17

soma pia


Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17

Wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 wakishangilia mara baada ya kuibuka mabungwa wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya kuifunga Guinea kwa mikwaju ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Mpoto Theatre kikitoa burudani kwa watazamaji wa fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyokutanisha Cameroon na Guinea hapo jana na Cameroon kutwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi ya penati 3 za Guinea.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Susan Mlawi wakati Naibu Waziri alipowasili  kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad wakati Naibu Waziri alipowasili  kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, kati ya Guinea na Cameroon jana jijini Dar es Salaam.
Vikosi vya timu za vijana chini ya miaka 17 toka Guinea na Cameroon wakiimba nyimbo za mataifa yao kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali hapo jana ambapo Cameroon waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi penati 3 za Guinea.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad (katikati) akimkabidhi bendera ya CAF Balozi wa Morocco Nchini Tanzania Abdelilah Benryane ikiwa ishara ya kuwa muandaaji wa mashindano hayo, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Wallace Karia.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi zawadi ya kombe mchezaji ambayealiibuka kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 jana jijini Dar es Salaam.
Washindi wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, timu ya Cameroon wakivalishwa medali mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad akimkabidhi nahodha wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 mara baada ya kuibuka mabingwa kwa ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.

Picha na WHUSM – Dar es Salaam



Hivyo makala Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17

yaani makala yote Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/matukio-mbalimbali-ya-fainali-za-afcon.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17"

Post a Comment