MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA

MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA
kiungo : MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA

soma pia


MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MASOKO makubwa zaidi  duniani yamepata nafasi ya kuwa vivutio kwa watalii na hiyo ni kutokana na bidhaa zinazouzwa katika masoko hayo pamoja na maonesho ya tamaduni mbalimbali, masoko makubwa na maarufu zaidi duniani ni pamoja na:

1. Soko la Tsukiji
Soko hili linapatikana Tokyo nchini Japan, ni soko kubwa la samaki duniani ni sehemu ambayo unaweza kupata vyakula freshi vya baharini pamoja na vinywaji.

Lilianza rasmi Februari 11, 1935 na huuza vyakula vya baharini zaidi ya 480 huku likiwa na migahawa na linafahamika zaidi kwa kuwa kivutio kwa wazawa na wageni.

2. Soko la Bazaar
Hili linapatikana  Instanbul nchini Uturuki, ni moja kati ya soko kubwa na kongwe zaidi duniani lililoanzishwa mwaka 1461. Ni kivutio kwa watalii na ni sehemu ambayo bidhaa za nguo,viungo na manukato hupatikana huku ikielezwa kuwa bidhaa zao ni bora zaidi.

Mwanzo soko hilo lilikiwa kituo cha biashara kwa ngome ya Ottoman ambapo soko hilo lilikuwa chini ya usimamzi wa wanajeshi wa nchi hiyo.

3. Soko la Chatuchak
Soko hili linapatikana Bangkong nchini Thailand likiwa ni soko kubwa zaidi nchini humo hasa kwa siku za mapumziko, soko hilo limechukua jumla ya hekari 35 pamoja ma stoo 15000 huku likiwa na sehemu za kuuza vyakula,nguo na mapambo. Hufunguliwa kila siku ila katika siku za mapumziko bidhaa hupatikana kwa wingi.

4. Soko la Marrackech Sooks
Hili hupatikana huko Marrakech nchini Moroccco, linapatikana katikati ya mji na limekuwa kitovu cha biashara pamoja masuala ya uchumi na tamaduni nchini humo.
Ni soko la kitamaduni na maarufu kwa kuuza bidhaa za ngozi, viungo na nguo na nyakati za jioni huwa soko la usiku ambapo vyakula mbalimbali kama kababu na vyakula vingine vya mtaani hupatikana na inaelezwa kuwa sehemu hiyo ni nzuri ya kufurahia usiku ukiwa nchini Morocco.

5. Soko la Viennese Krismasi
Soko hili linapatikana Vienna nchini Australia likiwa maarufu zaidi kwa kuuza bidhaa na mapambo ya krismasi, mishumaa, mapambo, vyakula na vinywaji hasa mvinyo.
Tamaduni za watu mbalimbali huoneshwa katika viwanja vya soko hilo zikiwemo kwaya za Krismasi huku likiwa na masoko makubwa zaidi ya 20.

6. Khan Al-Khalili
Hili linapatikana Cairo nchini Misri na lilianza karne ya 14 na lilianza kama kituo cha kuuzia dhahabu, viungo na madini mengine ya thamani na kwa sasa vito vya kila aina vinapatikana katika soko hilo pamoja na nakshi na mapambo ya kila aina. Soko hilo lina maduka  zaidi ya 900.
Ni soko ambalo limepakana na mji mkuu na ni moja ya soko kubwa na kongwe zaidi huku likiwa na sehemu ya kupumzika maarufu zaidi iitwayo Fishawi's Coffee iliyoanza kutoa huduma mwaka 1773.


Hivyo makala MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA

yaani makala yote MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/masoko-makubwa-na-maarufu-zaidi-duniani.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA"

Post a Comment