DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI

DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI
kiungo : DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI

soma pia


DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpongeza mwenyekiti wa halmshuri ya wilaya ya Iringa Vijijini Stephen Mhapa kumpa tuzo ya ngao kwa kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingira pamoja na kuwa na vyoo safi na bora.
Baadhi ya washiriki waliofika katika kikao hicho cha utoaji tuzo kwa utunzaji bora wa mazingira na kuwa na vyoo bora.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa sambamba na mkurugeni wa halmashauri ya Iringa vijijini Robert Masunya wakinywa maziwa ya Asas



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wananchi,viongozi,taasisi na jumuiya mbalimbali kwa kutekeleza vizuri kampeni ya kuwa na vyoo bora ambavyo vimeipa ushindi halmasahuri ya Iringa Vijijini kwa kupata tuzo ya usafi hapa nchini.

Kasesela alisema kuwa ofisi ya afya katika halmasahuri ya Iringa Vijijini wamekuwa wakisimamia vizuri swala la afya na kuwa na vyoo bora ambapo wanataraji kuwa halmashauri ya kwanza kwa kuwa na vyoo bora kuliko halmashuri zote za mkoa wa Iringa hadi taifa.

“Nampengeza bibi afya wa hapa amekuwa mkali kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kukwamisha zoezi lolote la kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hii wanakuwa na afya njema” alisema Kasesela

Aidha Kasesela amepiga marufuku wa wazazi kujifungulia majumbani kwa kuwa sio sehemu salama kwa uzazi wa mtoto wakati serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ambayo ndio kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano. 

“Jukumu la kwanza kwa baba ni kuhakikisha amempeleka mama kliniki kupata huduma ili kuwa na malezi mazuri ya mtoto,hivyo tutaondoa ile njia ya akinamama kujifungulia majumbani kwa kuwa tayari baba atakuwa anajua wajibu wake” alisema Kasesela

Kasesela amewataka watendaji wa kata,vijiji na maafisa tarafa kuhakikisha hakuna mama anajifungulia nyumbani na nitamshughulikia mtendaji yeyeto Yule ambaye hata wachukulia hatua akibaba watakao fanikisha mama kujifungulia numbani.

Awali akitoa hutuba kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa halmasahuri ya Iringa Vijijini Robert Masunya aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wameendeleza juhudi hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora ili kupunguza na kumaliza tatizo la milipuko ya magonjwa.

“Niwaombeni tena tuendelee kushirikiana vyema katika kuhakikisha halmasahuri ya Iringa Vijijini inaongoza kwa kuwa na mazingira bora na safi kuliko halmashuri zote hapa nchini kwa kuwa tuna mikakati ambayo ni bora sana” alisema Masunya


Hivyo makala DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI

yaani makala yote DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/dc-kasesela-marufuku-akina-mama.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI"

Post a Comment