title : RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI
kiungo : RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI
RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI
Ofisa madini mkazi wa kimkoa wa kimadini wa Simanjiro Daudi Ntalima akizungumza juu ya utaratibu wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani (maarufu kama ukuta wa Magufuli).
Wanawake wanaojihusisha na shughuli mbalimbali wakiwa kwenye mstari wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wanawake wachekechaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifanya kazi yao ya kuchekecha mabaki ya udongo unatolewa migodini.
………………………..
Ofisa madini mkazi wa kimkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima amepiga marufuku uuzwaji wa bia, viatu na wamachinga, pombe haramu ya gongo na vibanda vya uuzwaji baruti, ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani.
Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumzia utaratibu mpya wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi hiyo. Alisema utaratibu huo mpya utaanza kutumika April mosi mwaka huu na hakutakuwa na ruhusa ya watu kuingia na kukaa bila kazi maalum ndani ya ukuta huo.
Alisema migodi yote ndani ya ukuta inatakiwa kuzungushiwa uzio wa bati ndani ya miezi miwili na migodi au leseni ambazo hazifanyiwi kazi zitafutwa.
“Vibanda au makazi yoyote nje ya uzio wa mgodi husika hayaruhusiwi tena na hairuhusiwi kukata mti wowote ndani ya ukuta bila kibali,” alisema Ntalima. Alisema hairuhusiwi mtu yeyote kuonekana maeneo ya machimbo tofauti na maeneo ya masoko bila kibali na vibanda au makazi yoyote nje ya uzio wa mgodi hayaruhusiwi.
Alisema maeneo mapya ya masoko yaliyotengwa kwa kupewa namba maalum ya kufanya biashara wanapaswa kuwa na kitambulisho cha mjasiriamali. “Watu wote wanaofanya biashara mbalimbali ndani ya ukuta tofauti na uchimbaji madini wanapaswa kufuata utaratibu huu mpya uliotolewa,” alisema Ntalima.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Mirerani, walipongeza hatua hiyo kwani siyo vyema kwa kila mtu anapaswa kuingia ndani ya ukuta hadi migodini. Hassan Juma alisema hivi sasa kuna watu wengi kwenye maeneo ya migodini huku huduma za vyoo ikiwa ni tatizo hivyo kuhofia magonjwa ya milipuko pindi mvua zikinyesha.
Kaanael Minja alisema biashara nyingine ambazo hazina umuhimu wa kuwepo ndani ya ukuta zinapaswa kukomeshwa hasa wamachinga na wanawake wanaojiuza kwa wanaApolo. “Watu ni wengi migodini vumbi la ulanga linatimka na kuhofia ugonjwa wa Silikosis pia baada ya watu kuruhusiwa kuna wanawake wanaojiuza migodini,” alisema Minja.
Hivyo makala RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI
yaani makala yote RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/rmo-simanjiro-atoa-utaratibu-mpya.html
0 Response to "RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI"
Post a Comment