ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU
kiungo : ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

soma pia


ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mipango, Ufutuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kulthumu Mansoor amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi ya uhujumu ambapo anadaiwa kujipatia zaidi ya sh. bilioni 1.4 kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka kwa wafanyakazi wenzake. Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kelvin Mhina kuwa katika tarehe tofauti za Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya tarehe 13 Agosti 2003 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu imedaiwa, kati ya Januari 2012 na Mei 2017 huko Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Saalam mshtakiwa kwa kudanganya alijipatia jumla ya sh. milioni 32.2 kutoka kwa watu sita tofauti tofauti kama malipo ya viwanja tofauti vilivyoko Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Ukuni kwa kujifanya kuwa yeye ni mmliki wa kiwanja viwanja hivyo huku akijua kuwa sio kweli.

Mshtakiwa anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka kwa Alex Mavika ( milioni Sh.5.2), Wakati Katondo, (milioni 3), Gogo James, (milioni Sh.5), Ekwabi Majungu, (Sh.milioni 7) John Amos (Sh.milioni 7) na Rose Anatory, (Sh.milioni 5), ambao wote ni wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Katika shtaka la mwisho imedaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko Upanga, mshtakiwa Kulthumu alijipatia fedha Sh.1,477,243,000 wakati akijua kuwa fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa Tangulizi la kughushi.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 12, 2019
 ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kulthumu Mansoor akiwa kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  akikabiliwa na kesi ya uhujumu ambapo anadaiwa kujipatia zaidi ya sh. bilioni 1.4 kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha 
 ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kulthumu Mansoor akifikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi ya uhujumu ambapo anadaiwa kujipatia zaidi ya sh. bilioni 1.4 kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha 


Hivyo makala ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

yaani makala yote ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/aliyekuwa-bosi-takukuru-afikishwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU"

Post a Comment