title : WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM
kiungo : WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM
WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Sulemani Jafo amesema ndoto yake ni kuona eneo la bonde la Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu sasa linaboreshwa na kuwa eneo ambalo litakuwa kivutio.
Ametoa kauli hiyo leo Februari 25,2019 wakati anazungumza na maofisa wa ngazi mbalimbali wa Benki ya Dunia ambao wapo nchini na leo na kesho watakuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya Jiji hilo ikiwemo ya miundombinu ambapo amesema Dola milioni 100 zinahitaji kwa ajili ya kuboresha bonde hilo na hivyo ametoa ombi kwa benki hiyo.
Amefafanua katika bonde la Mto Msimbazi zipo familia ambazo zimepoteza wapendwa wao kutokana na kufa maji kutokana na mafaruko ambayo yamekuwa yakitokea wakati wa msimu wa vua, hivyo anachotamani ni kuona kero iliyopo bonde la Msimbazi inatatuliwa na kubaki eneo salama na kivutio.
"Mimi ni Waziri ni mdogo na ukweli ndoto niliyonayo ni kuona kero ya bonde la Mto Msimbazi inaondolewa na kubaki eneo salama ambalo litakuwa kivutio. Dola Milioni 100 zinahitajika kukamilisha mradi wa kuboresha bonde hilo.Ni matumaini yangu Benki ya Dunia mtashirikiana nasi kama ambavyo tunashirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema Waziri Jafo.
Eneo hilo la msimbazi kupitia mradi huo wa uborshwaji wa eneo hilo litakuwa kivutio kutokana namna ambavyo utajengwa kwa kuwa na maeneo ya kupumzika na kubwa zaidi mandhari yake itavutia watu wengi.
Maofisa hao wa Benki ya dunia ambao kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi ambayo wanaifadhili, walifika ofisi za TAMISEMI ambapo Waziri Jafo ametoa shukrani kwa benki hiyo kwa namna ambavyo inatoa fedha kwa ajili ya kufanikisha uboreshaji wa sekta mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara,majiji nane,elimu,afya na sekta nyingine.
Wakati huo huo Waziri Jafo amezungumzia namna ambavyo maeneo mengi ya nchi yetu yameboreshwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia."Benki hii imetoa Sh.trilioni mbili kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika majiji nane pamoja na uboreshaji wa maeneo mengine.
"Kwa namna nchi yetu ilivyojenga Watanzania ambao wameondoka miaka 10 iliyopita wakirudi leo hii wanaweza kupotea kwenye baadhi ya mitaa,kwani imeboreshwa sana.Hata yale maaneo ambayo yalikuwa hayapiti leo hii yana barabara na yanapitika vizuri.Ukweli mitaa mingi imeboreshwa."
Amewaambia maofisa wa Benki ya dunia kuwa Serikali ya Tanzania inatoa shukrani nyingi kwa benki hiyo na kubwa zaidi inatambua namna ambavyo inathamini mchango wao wa kusaidia uboreshaji wa sekta mbalimbali.
Kuhusu ziara ya maofisa hao,amewaambia kuwa watapata fursa ya kuona namna miradi mingi iliyotekelezwa na ile ambayo bado ipo katika hatua mbalimbali kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam(DMP).
"Mtapata fursa za kuona namna ambavyo Jiji la Dar es Salaam lilivyoboreshwa kupitia miradi ya DMP.Tunashukuru kwa ushirikiano wenu Benki ya dunia,tuendelee kushirikiana.Rais wetu Dk.John Magufuli ametoa maelekezo Makao makuu ya Serikali yawe Dodoma na Jiji la Dar es Salaam liwe la kibiashara .Hivyo tunaka kuona Jiji hili linavutia kibiashara," amesema Waziri Jafo.
Kwa upande wao maofisa wa Benki ya Dunia wamemwambia Waziri Jafo kuwa wamefurahishwa na namna ambavyo utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wanaendelea kusaidia fedha za miradi ya maendele
Hivyo makala WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM
yaani makala yote WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/waziri-jafo-asema-dola-milioni-100.html
0 Response to "WAZIRI JAFO ASEMA DOLA MILIONI 100 ZAHITAJIKA KUBORESHA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJI LA DAR ES SALAAM"
Post a Comment