WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA

WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA
kiungo : WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA

soma pia


WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA

Kila jambo jemba huanza ni dua au sala, kabla ya kuaza kwa zoezi la upandaji miti, watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mafanya maombi mafupi kumwomba Mungu aikuze miti hiyo. Pichani watumishi wakiwa wameinamisha vichwa kumwomba Mungu ashushe baraka zake katika kazi yao.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dr. Evaristo Longopa akipanda mti aina ya Ashok wakati zoezi la upandaji miti kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Jumla ya miti 75 ilipandwa katika eneo linalozunguka kiwanja inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika Mji wa Serikali huko Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Dr. Longopa alitoa wito kwa watumishi hao kuwa wasiishie kupanda tu bali pia kuitunza ili ikue na kupendezesha mandhari ya Ofisi na kuhifadhi mazingira.
Watumishi wakiwa wametawanyika wakiendelea na zoezi la kupanda miti aina ya Ashok na Miti Dodoma katika kwanja panapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zaidi ya miti 600 ikiwamo ya matunda inatarajiwa kupandwa katika eneo hilo.
Baada ya kupanda miti Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwaongoza watumishi katika kuangalia kazi ya ujenzi wa Ofisi yao ilivyokuwa ikiendelea. Pichani Naibu Mwanasheria Mkuu akiongozwa na Injinia Suma Atupele kukagua kazi ya ujenzi inavyoendelea.
Naibu Mwanasheria Mkuu akiangalia mabati yatakayotumika kuenzekea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku Injia Suma Atupele akitoka maelezo


Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dr. Evaristo Longopa amewataka watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakisha kwamba, miti waliyoipanda leo inatunzwa ipasavyo na kukua ili ipendezeshe mandhari ya Ofisi na kuhifadhi mazingira. 

Dr.Longopa ametoa wito huo leo, Ijumaa, wakati alipowaongoza watumishi wa Ofisi yake katika zoezi la upandaji miti, katika kiwanja inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mji wa Serikali huko Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma. 

Miti ambayo imepandwa katika zoezi hilo ni 75 kati ya 640 inayotarajiwa kupandwa katika eneo hilo. Miti hiyo 75 ni aina ya Ashoki na Miti Maji au maarufu kama miti Dodoma imepandwa kama sehemu ya mpaka wa kiwanja cha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

“Watumishi wenzangu, leo tunazindua zoezi la kupanda miti 75 kati ya 640 ikiwamo ya matunda ambayo tutapanda katika eneo letu. Upandaji huu wa miti unayo malengo tuseme mawili, kwanza kupendezesha mandhari ya eneo la Ofisi yetu ili yawe ya kuvutia na pili ni kuhifadhi mazingira. Niwatake basi tusiishie kupanda tu bali kila mmoja wetu ahakikishe anatunza miti hii ili iweze kukua na kustawi”. Akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu kuongoza na kushiriki zoezi hilo, wangine walioshiriki ni pamoja na Mkurugenzi wa Mipango Bi. Nkuvililwa Simkanga na Bw. Jackson Nyamihula ambaye n Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu. 

Kwa upande wao watumishi hao wakionesha kufurahia zoezi hilo la upandaji miti, baadhi walipendekeza kwamba kila aliyepanda mtu aweke alama yake ili kuhakikisha kwamba kila mmoja anautunza mti wake. 

Baada ya zoezi la upandaji miti, Naibu Mwanasheria Mkuu alikwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ambapo mmoja wa ma – Injinia anayesimamia ujenzi huo Injinia Suma Atupele alimweleza Naibu Mwanasheria Mkuu kwamba kazi inaendelea vizuri ambapo kazi mbalimbali zikwamo za uchapiaji na upakaji rangi na nyinginezo nyingi zimekuwa zikiendelea kwa kasi ya kuridhisha. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 
Dodoma


Hivyo makala WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA

yaani makala yote WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/watumishi-ofisi-ya-mwanasheria-mkuu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATUMISHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WATAKIWA KUTUNZA MITI WALIYOIPANDA"

Post a Comment