title : Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba
kiungo : Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba
Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba

Inakadiriwa kwamba asilimia 16 ya Watanzania (Watu wazima) ambayo ni sawa na watu milioni 4.4 wengi wao wakiwa ni wanawake, wameungana na kuanzisha Zaidi ya vikundi 50,000 vya kuweka na kukopa pesa vijulikanavyo kama Vicoba na vikiwa vimekusanya fedha taslimu zaidi ya Shilingi bilioni 100 za Kitanzania
Kama kiongozi katika soko la mfumo wa pesa za simu, Vodacom M-Pesa, ilizindua na kubuni njia mbali mbali ambazo zinakidhi mahitaji ya soko na kuwavuta wateja wake katika mfumo wa kidigitalli, hivyo huduma ya Vodacom Pamoja Group Savings imelenga katika kufanikisha hili.
“Naamini kwamba kila mmoja wetu anatambua au amejiunga katika SACOSS, Kikoba au upatu. Vodacom inatambua umuhimu wa vikundi hivi katika kuinua vipato vya watu mbali mbali katika jamii, ndio maana tumetengeneza huduma hii ili kuvifanya vikundi hivyo kuwa fanisi zaidi, lakini pia kuwavuta katika huduma za kifedha za kidijitali” alisema Mkurugenzi wa M-Commerce, Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni.
Huduma hii imelenga kutatua matatizo ambayo vikundi hivi vimekuwa vikikumbana nayo kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na usalama, utunzaji wa taarifa, ukusanyaji wa fedha pamoja na ugawaji wa faida ipatikanayo kwa hisa ambazo wamekuwa wakijiuzia ndani ya vikundi hivi. hivyo basi itawawezesha familia, marafiki na vikundi vya upatu kupata huduma za kifedha kwa usalama zaidi na muda muafaka.
Kwa kutumia Pamoja Group Saving washiriki wote wa makundi wataweza kufuatilia mwenendo mzima wa kifedha wa kundi, ikiwemo kiasi cha fedha kilichopo ndani ya kundi. Huduma hii ni ya kipeekee na unaongeza uwazi na kupunguza ugumu na utofauti katika uongozaji wa vikundi, Huduma hii itakuwa kwa wateja wote wa Vodacom pale itakapozinduliwa na itatumika na vikundi vyote vya fedha.
Hivyo makala Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba
yaani makala yote Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/vodacom-tanzania-yajipanga-kuzindua.html
0 Response to "Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba"
Post a Comment