Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula.

Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula.
kiungo : Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula.

soma pia


Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula.

Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Tanzania, Bi Rosalynn Mworia (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Vodacom Foundation Tanzania kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi. 
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Tanzania, Bi Rosalynn Mworia (kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Vodacom Foundation Tanzania kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. Wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi. 
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia (kulia) akisalimiana na baadhi ya wagonjwa wanaopata matibabu ya Fistula mara baada ya kuwasili kwenye Hospitali ya CCBRT wakati wa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. 



Katika kuunga mkono na kuongeza nguvu juhudi za kutokomeza fistula nchini, Taasisi ya Vodacom Tanzania Faundation kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT wametoa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa vituo vya afya na wadau mbalimbali kutoka ofisi za serikali. Programu hii ya “Fistula inatibika” ilianza mwaka 2012 na imelenga kuwasaidia wanawake wanaoishi na hali ya fistula kupata matibabu ya kiafya na kisaikolojia kwa sababu wengi wao hutengwa na jamii zinazowazunguka kutokana na ugonjwa huo, pamoja na kuwawezesha kurejea katika hali zao za kawaida na kujumuika kwenye jamii zao. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia alisema, “Mabalozi hawa wanaungana na mabalozi wengine zaidi ya 3000 wa fistula waliopo sehemu mbalimbali nchini, wenye uwezo wa kutambua na kuwawezesha waathirika wa Fistula kufika hospitali ya CCBRT au vituo vingine vya afya vinavyotoa matibabu hayo kama; Bugando (Mwanza), KCMC (Kilimanjaro), Nkinga (Tabora), Peramiho Mission Hospital (Ruvuma), Kabanga Mission Hospital (Kigoma), Songea Regional Hospital (Ruvuma) na Selian (Arusha) kwa kutumia mfumo wa M-Pesa. Nawasihi mabalozi hawa kutoa mafunzo kwa jamii zao kuhusu fistula kwa kuandaa semina ambazo zitaambatana na majadiliano ya changamoto mbali mbali zinazotokana na fistula”. 

Shirika la Afya duniani (WHO) linakadiria kwamba wanawake 3000 hupata tatizo la fistula kila mwaka nchini Tanzania. Hivyo mpango huu ulianzishwa na Vodacom Tanzania Foundation kama sehemu ya kuisaidia serikali kuboresha huduma za afya nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

“Fistula ni hali inayozuilika na kutibika hivyo inabidi tuidhibiti kabisa. Katika karne hii hakuna mwanamke anayestahili kutengwa au kunyanyapaliwa na jamii yake kwa sababu ya fistula. Ninapongeza juhudi za taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation katika kukabiliana na matatizo ya kiafya yatokanayo na uzazi nchini. Tunahitaji kukabiliana na mzigo huu wa akina mama wenye matatizo haya katika jamii zetu,” alisema Afisa Mtendaji mkuu wa hospitali ya CCBRT bi Brenda Msangi. 

Wanawake wenye fistula wana changamoto kubwa ya kutengwa katika jamii zao na wengi wao hawatambui kama hali hii inatibika kutokana na ukosefu wa elimu na taarifa. Utumiaji wa mabalozi wa Fistula ni hatua muhimu zaidi maana wao hutumika katika kuwatambua na kuwapa rufaa wanawake wanoishi na hali ya Fistula 

“Mwaka wa kwanza baada ya kuanza kutumia M-pesa kutoka Vodacom katika mfumo wetu wa rufaa tulishuhudia ongezeko la asilima 65 ya wanawake waliotibiwa ugonjwa wa fistula, kufikia mwaka 2016, asilimia 87 ya wagonjwa wa fistula walipata rufaa kupitia mfumo wa M-Pesa ambao tunashirikiana na Vodacom Tanzania Foundation, wakafanikiwa kufika CCBRT ambapo tulifanya upasuaji wa wagonjwa 1,012”, aliongeza Bi Msangi.


Hivyo makala Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula.

yaani makala yote Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/vodacom-ccbrt-waungana-kutokomeza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula."

Post a Comment