UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO

UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO
kiungo : UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO

soma pia


UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO

Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akielezea namna chumba cha ICU kinavyowahudumia wagonjwa waliotoka katika chumba cha upasuaji kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiongea jambo na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama mwenye ndoto ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alipotembelea taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya wakizungumza na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo ziara. Picha na JKCI .


UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wameishauri Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kufuatilia na kulea vipaji vya watoto wenye ndoto ya kuwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa siku zijazo.

Rai hiyo imetolewa hospitalini hapo leo na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Rashid Semindu, wakati walipofanya ziara wakiwa wameambatana na Maria Manyama ambaye ni msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Mitihani la Taifa.

“Tunaipongeza serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika taasisi hii”.

“Tunawapongeza nanyi wafanyakazi wa Taasisi hii kwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo mkubwa kusaidia watanzania na wagonjwa wengine ambao mmetueleza huwa wagonjwa wengine mnawapokea kutoka nje ya nchi, kwa kweli mnafanya kazi kubwa na nzuri,” alisema.

Ameongeza, “Tunao vijana wengi ambao wana ndoto ya kuwa madaktari bingwa kama ambavyo Maria ametueleza ndoto yake, vijana wa chipukizi, tunaomba JKCI muwalee ili waweze kufikia ndoto zao hizo, kwani hii ni hazina ya Taifa letu.

Akizungumza, Maria amesema alidhamiria kusoma udaktari na kubobea katika masuala ya moyo tangu alipokuwa akisoma mkoani Mbeya.

“Tulipofanya ziara za kimasomo katika hospitali mbalimbali, nilikuwa nashuhudia jinsi ambavyo watanzania wenzangu wakubwa kwa wadogo wanavyoteseka kwa kuugua magonjwa haya.

“Nikaweka bidii katika masomo yangu, namshukuru Mwenyezi Mungu amenisaidia nimefanya vizuri, nawashukuru wazazi wangu kwa kuniwezesha kila hatua, walimu wangu kwa kunifundisha kwa moyo na wanafunzi wenzangu kwa ushirikiano wao,” amesema.

Baba mlezi wa Maria, Leonard Manyama amesema matokeo ya binti huyo yaliwashangaza. “Alianza kutueleza juu ya ndoto yake ya kuwa daktari kabla hata hajafanya mtihani, alianza kutafuta shule ya kwenda kusoma kwenye mtandao, akasema Feza Sekondari itamfaa, tukaendelea kumfuatilia kwa ukaribu, matokeo yake yalipotoka tulistaajabu, amefaulu kwa kiwango cha juu na Feza wamekubali kumsomesha bure,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Delila Kimambo amempongeza msichana huyo kwa kuamua kutembelea taasisi hiyo kujifunza.

“Nimekubali kuwa mlezi wake, nitamsaidia popote pale atakapokuwa akihitaji msaada ili aweze kufikia ndoto yake,” alisema Dk. Kimambo.


Hivyo makala UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO

yaani makala yote UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/uvccm-waishauri-taasisi-ya-moyo-jakaya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO"

Post a Comment