title : TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam
kiungo : TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam
TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt Edwin P.Mhede akiongea na wadau wa Zao la Muhogo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Zao la Muhogo ulioratibiwa na TanTrade na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Zao la Muhogo wakiwa kwenye Mkutano wa wadau wa Zao la hilo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
Mama MWANTUMU MAHIZA akizungumza na Wadau wa Muhogo baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania
Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania Bw.Burton Mwankuru Nsape(Kushoto) akiwa na Katibu Msaidizi Bw.Victor Vedasto Kabegu(Kulia)
Afisa Masoko wa Kampuni ya EADL kwa kushirikia na TAEPZ akitangaza kununua Zao la Muhogo wakati wa mkutano na wadau wa zao hilo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania chenye lengo la kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano wa Wadau wa Zao la Muhugo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo Bi Upendo Mndeme akizungumza kwenye mkutano wa mkutano wa wadau wa Zao la Muhogo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………….
Wazalishaji wa Zao la Muhogo nchini wameshauriwa kuzalisha zao hilo kitaalam, kwa ubora, kiwango kinachohitajika kwenye soko na kwa kutumia mbegu bora inayozalisha mavuno mengi.
Rai hiyo imetolewa na Dkt Edwin P.Mhede Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Zao la Muhogo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
“Wengi mnafahamu kuwa changamoto katika zao hili ni upatikanaji wa mbegu bora, aina ya mbegu inayoweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha uhaba wa upatikanaji wa mavuno ya kutosha na uzalishaji mdogo unaochagizwa na kilimo cha mashamba madogo madogo” alisema Mhede
Alisisitiza kwa kuiomba Wizara ya Kilimo na Vituo vya Utafiti vya Kilimo kuendelea kutafiti juu ya changamoto hizi na kuimarisha huduma za ugani zenye kulenga uzalishaji wa tija ili kupata mazao mengi zaidi.
Aliongeza kwa kusema kuwa kwa muda mrefu zao hili lilikuwa linategemewa kama zao la chakula pekee lakini kutokana na maendeleo ya uchumi na teknolojia kukuaa katika nchi zinazoendelea zimekuwa zikitumia Zao la Muhogo kutengenezea wanga ambao unatumika kwa matumizi mbalimbali viwandani vikiwemo viwanda vya karatasi, vinywaji na bidhaa kama nguo na makaratasi na kwa nchi nyingine wanatumia kuzalishia nishati mbadala aina ya Ethanol na kuzalisha sukari ya viwandani yenye ubora wa juu.
Naibu Katibu Mkuu aliendelea kusema kuwa Zao la Muhogo ni zao rasmi la biashara hivyo linasaidia katika kuongezea pato la taifa. Kwa takwimu zilizopo katika kipindi cha mwaka 2015/16 Zao la Muhogo lilichangia asilimia 13.63 ya pato la taifa huku likiajiri wakulima wadogo zaidi ya milioni 1.3 Kati ya mwaka 2012 na 2016 kiasi cha tani 59,447,754 za Muhogo chenye thamani ya Dola za Marekani 4,804,926 uliuzwa nje ya nchi.
Kwa upande wa masoko serikali inaendelea kuimarisha mfumo mzuri ambao utasaidia upatikanaji wa masoko hasa nje ya nchi. Zipo hatua zilizofanyika kwa nchi kama ya China yenye uhitaji wa Zao hilo kwa kuwa na mikataba ya pamoja uliohusu punguzo la ushuru wa forodha kwa bidhaa za Tanzania kuingia soko la China, mkataba wa itifaki ya Muhogo wa namna ya uingizaji wa zao hilo nchini China na kupitia mahusiano kati ya nchi na nchi. Na matokeo ya juhudi hizi zimeonekana kwa makampuni mbalimbali kutoka China kama vile Epoch Agriculture, Foshang Guangji Co. Ltd na Dar Canton Co Ltd zinazojishughulisha na ununuzi wa Muhogo na zikijiandaa kwa ujenzi wa viwanda nchini.
Nae Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi wa TanTrade alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto zinazolikabili Zao la Muhogo ili kujua jinsi ya kulikabili ingawa changamoto kubwa katika uzalishaji wa Muhogo ni namna ya kuliongezea thamani ili kuepuka changamoto za kimasoko
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa TanTrade itasimamia uanzishwaji na usajili wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania, lengo ni kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo. Chama hicho kitakuwa chini ya uangalizi wa TanTrade na makao makuu yake yatakuwa katika ofisi za TanTrade.
Bi Upendo Mndeme Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo amewashauri wazalishaji wa Zao la Muhogo ili liwe la Kibiashara hasa katika nchi ya China lazima wazingatie vigezo vilivyoainishwa katika itifaki ya soko la Muhogo ambapo baadhi ya vitu ni bidhaa za Muhogo zisiwe na visumbufu vya wadudu na magojwa, wazalishaji na makampuni ya kuuza Muhogo nchini China kutambulika Kisheria, ubora wa bidhaa, bidhaa zifungashwe kulingana na matakwa ya soko la China, ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuvuna na Wizara ya Kilimo au Kampuni/ Taasisi iliyopata kibali cha Wizara kwa ajili ya kazi hiyo n.k
Baadhi ya Viwanda vya ndani vilivyojitokeza kununua Zao la Muhogo wamethibisha utoshelezi wa soko la ndani na uhitaji wao wa Zao hilo na wamehakikisha kuwa watalipandisha thamani Zao hilo kabla soko la nje kuwa na uhitaji mkubwa zaidi
Hadi sasa mikoa inayozalisha Muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Lindi, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Kigoma
Hivyo makala TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam
yaani makala yote TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/tantrade-yawashauri-wazalishaji-wa-zao.html
0 Response to "TanTrade yawashauri wazalishaji wa zao la Muhogo kuzalisha kitaalam"
Post a Comment