Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba

Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba
kiungo : Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba

soma pia


Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba

Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar 15.02.2019
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Shirika la Bandari limeanza kuweka Mashine ya ukaguzi katika Bandari ya Mkoani Pemba na inategemea kuweka katika Bandari zote zilizobakia.
Hatua hiyo ina lengo la kuendeleza kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuwakagua Abiria na Mizigo yao ili nchi iendelee kuwa salama.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Muhammed Ahmada Salum ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake Suleiman Sarahan Said katika Kikao cha Baraza kinachoendelea.
Amesema kwa mujibu wa Kanuni za Kimataifa za ulinzi na usalama “International Ships and Port Facility Security Code” (ISPS Code), maeneo ya kuingia na kutoka nchini kama bandarini kunatakiwa kukaguliwa abiria na mizigo yao ili kuhakikisha abiria, mizigo na miundombinu ya bandarini pamoja na meli zipo hali ya usalama.
Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa Wizara kupitia Shirika la Bandari imeanza kutekeleza kanuni hizo kwa kuweka mashine za ukaguzi wa Abiria na Mizigo kwa Bandari ya Unguja kwa abiria wanaotoka na kuingia Unguja na Dar es salaam na kwa upande wa Pemba wameweka katika Bandari ya Mkoani.
Amefahamisha kuwa utaratibu wa zoezi hilo umeleta mafanikio ya uhakika katika ulinzi na usalama kwa abiria na mali zao katika vyombo wanavyopanda.
Hata hivyo amesema Serikali inaandaa mikakati ya kuweka Mashine katika Maeneo yote ya Bandari kwani mashine moja iliyopo katika Bandari ya Mkoani haitoshelezi kulingana na wingi wa abiria.
Hivyo Naibu Waziri huyo amesema kutokana na abiria wanaosafiri kuwa wengi kwa wakati mmoja Shirika la Bandari limedhamiria kuweka Mashine ya pili ili kuondosha msongomano wa abiria wakati wa kupanda na kushuka Meli.


Hivyo makala Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba

yaani makala yote Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/serikali-kuweka-mashine-ya-ukaguzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Serikali kuweka mashine ya ukaguzi Bandari ya Mkoani Pemba"

Post a Comment