title : SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB
kiungo : SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB
SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SAFARI ya treni ya wasanii mbalimbali imenoga!Hicho ndicho ambacho unaweza kukizungumzia baada ya wasanii hao zaidi ya 300 kupata fursa ya kupanda treni kwa lengo la kuhakikisha wanashuhudia ujenzi wa reli ya kisasa ambayo itatumia umeme (SGR).
Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli ambapo reli hiyo pamoja na mambo mengine itasaidia kuinua uchumi wa nchi yetu.
Wasanii hao wameondoka jijini Dar es Salaam leo Februari 7,2019, saa tatu asubuhi kuelekea mkoani Morogoro ambapo wakiwa katika safari hiyo watashuhudia hatua mbalimbali za mbalimbali za ujenzi huo.
Wakizungumzia safari hiyo leo kwa nyakati tofauti wasanii hao kila mmoja ameelezea furaha aliyonayo na hasa kuwa sehemu ya watanzania waliobahatika kushuhudia ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.Kiongozi wa msafara huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Staa wa filamu nchini katika tasnia ya 'Bongo Muvi' Steven Jacob a.k.a Jay B amesema kuwa anajisikia fahari kusafiri na treni ya ndani kwenda kushuhudia ujenzi wa reli ya kisasa. "Leo ni mara yangu ya kwanza kupanda usafiri huu wa treni kwa hapa nyumbani kwetu ila nikiwa China nimewahi kupanda treni inayotumia umeme."
Ameongeza ni matumaini yake kwenye safari hiyo kuna mambo mengi atajifunza na kuwa balozi mzuri wa kuwaambia Watanzania wengine kuhusu ujenzi wa reli hiyo.Wasanii wengine ambao wamezungumzia safari hiyo wamesema wanampongeza Rais Dk.John Magufuli kutokana na jitihada ambazo anafanya katika kuleta maendeleo ya Watanzania.
Kwa upande wake msanii Steven Nyerere wakati anazungumzia safari hiyo ameeleza kuna mambo mengi ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na hivyo ni vema wasanii wakawa sehemu ya mabalozi kwanza kwa kutembelea miradi hiyo na kisha kuielezea vema.
"Huu ni mwanzo tu, kwani kutokana wingi wa miradi ambayo inafanywa na Serikali chini ya Rais wetu Dk.John Magufuli naamini tutapata fursa ya kushuhudia mradi mmoja baada ya mwingine.Nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwa Rais kwa hatua anazochukua katuka kuleta maendeleo nchini kwetu.Wasanii tunaahidi kumuunga mkono kwa kila jambo analofanya kwa maslahi ya Waanzania wote,"amesema Steven Nyerere.
Hivyo makala SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB
yaani makala yote SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/safari-ya-wasanii-kuangalia-ujenzi-wa.html
0 Response to "SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB"
Post a Comment