title : RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON.
kiungo : RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON.
RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae amepewa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Africa (AFCON) leo amezindua rasmi kamati hiyo yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.
RC Makonda amesema majukumu makubwa 3 watakayoanza nayo Kama kamati ni Kuirudisha timu kwa wananchi, kuweka maandalizi mazuri ya timu na uwezeshaji wa timu.
Aidha RC Makonda amesema katika kikao cha Leo kamati imepanga kukutana na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Wasanii, Wanasiasa, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na wadau mbalimbali ili kwa pamoja tuiunge mkono timu ya Taifa.
Hata hivyo RC Makonda amesema kwa sasa timu ipo katika mikakati ya maandalizi ya Mechi ya mwisho dhidi ya Uganda itakayochezwa Machi 24.
Kamati hiyo inaongozwa na RC Makonda ambae ni Mwenyekiti, Katibu wake akiwa ni Mhandisi Hersi Said ambapo Wajumbe wa kamati hiyo ni Mohamed Dewji, Haji Manara, Jerry Muro, Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Tedy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid na Faraji Asas.
TAIFA STARS TUNA KILA SABABU YA KUSHINDA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Africa (AFCON) ,ambapo leo amezindua rasmi kamati hiyo yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.
Hivyo makala RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON.
yaani makala yote RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/rc-makonda-ataja-silaha-3-atakazotumia.html
0 Response to "RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON."
Post a Comment