title : MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI
kiungo : MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI
MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Mwambawahabari
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) amepongeza jitihada za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa za kujikwamua kiuchumi kwa kutumia vizuri fedha za TASAF.
Pongezi hizo amezitoa wakati wa mkutano kati yake na wakazi wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.
Mhe. Mkuchika ametoa pongezi hasa kwa kinamama kwa kutumia vizuri fedha hizo katika kuzalisha miradi ya maendeleo na amefurahishwa na ushuhuda wa akina mama ambao mwanzoni walitumia vibaya fedha hizo lakini baadae wakawekeza katika miradi ya maendeleo.
Mhe. Mkuchika ametoa ufafanuzi kuwa lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kupambana na umaskini ili kuboresha hali duni za Watanzani na kuagiza wanufaika wa TASAF kutofanyia mzaha fedha wanazozipata.
Aidha, Mhe. Mkuchika amepongeza wasimamizi wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Mratibu wa TASAF wa halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Akitoa ushuhuda katika mkutano huo, mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi wa kijiji cha Mkwanyule, Bi. Mwanahamisi Ukwenda, ameishukuru serikali kwa kuianzisha TASAF kwani imemuwezesha kufanya shughuli za ufugaji wa kuku na mbuzi na kupata fedha ambazo zinamsaidia kwa mahitaji maalumu mara anapouza mifugo hiyo.
Aidha, Bi. Mwanahamisi amekiri kutotumia vizuri fedha za TASAF alizozipata katika awamu ya kwanza na ya pili na kuahidi kuendelea kuzitumia vizuri fedha hizo kwa sasa.
Mnufaika mwingine, Bw.Hassan Charahani ameushukuru mradi wa TASAF kwa kumkwamua kwenye umaskini kwani hapo awali alikuwa akila mlo mmoja kwa siku na hakuweza kusomesha watoto lakini TASAF imebadili maisha yake.
Kwa upande wake Mbunge wa Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha wakazi wa kijiji cha Mkwanyule kuwa na miradi ya ufugaji kuku, mbuzi na kujenga bwawa la maji na pia ameipongeza serikali kwa kutokua na ubaguzi katika kuleta maendeleo nchini kwa kuwa Mkwanyule inaongozwa na viongozi wa chama cha CUF.
Mhe. Mkuchika anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Lindi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.
Hivyo makala MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI
yaani makala yote MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mhemkuchika-apongeza-wanufaika-wa-tasaf.html
0 Response to "MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI"
Post a Comment