title : MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU
kiungo : MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU
MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amelihakikishia Bunge kuwa Serikali inayo nia njema kwa watumishi wote wa umma kwa kuhakikisha wanapata mishahara yao na stahiki zote ambazo wanastahili kulipwa na kwamba mchakato uliopo sasa ni kuangalia kwa kina namna ya kuboresha maslahi yao.
Akijibu swali bungeni leo Februari 7, 2019 , Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imekuwa na mipango mbalimbali na kwamba nia ya Serikali ni njema kwa kuhakikisha watumishi wanalipwa stahiki zao kwa wakati.
Ametoa ufafanuzi huo baada ya moja ya wabunge kutaka kufahamu ni lini Serikali itaongeza mishahara ya watumishi ambayo ni haki yao kisheria na si takwa la mtu.Hivyo wakati anajibu swali hilo ametumia nafasi hiyo kufafanua dhamira ya Serikali kwa watumishi wa umma ambapo pamoja na mambo mengine ameleeza wazi kila mtumishi lazima apate stahiki yake.
Pia amesema kabla ya kupandishi mishahara kumukuwepo na hatua mbalimbali ambazo zinazchukuliwa na baadhi ya hatua hizo ni kufanya uhakiki wa watumishi baada ya kubainika uwepo wa watumishi hewa ambao walikuwa wanalipwa mishahara na posho.Ameongeza hatua ya pili ikawa ni kuhakiki vyeti na baada mchakato huo Serikali ikawa inalipa na madeni.
"Kuna hatua mbalimbali ambazo Serikali imechukua katika kuhakikisha mishara inakwenda kwa watu wanaostahili.Pia kwa sasa kuna tume ambayo inaendelea kufuatilia mishahara kati ya kada moja na nyingine ambayo hiyo itatoa picha halisi ya viwango vya mishahara kulingana na kazi ambayo inafanywa eneo husika.
"Kumekuwa na toauti kubwa ya mshahara wakati mfanyakazi wa eneo husika amesoma chuo kikuu kimoja na mwingine lakini linapokuja suala la mshahara tofauti inakuwa kubwa.Hivyo yote hayo tume hiyo inaangalia na kisha itakuja na mapandekezo kuhusu viwango vya ishahara.Niwahakikishie wabunge na Watanzania nia ya Serikali ni njema,"amesema Waziri Mkuu.
Hivyo makala MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU
yaani makala yote MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mbunge-aibana-serikali-nyongeza-ya.html
0 Response to "MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU"
Post a Comment