title : MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI
kiungo : MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI
MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bi. Vicky Mbunde akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo Mjini Musoma.
Katibu Tawala msaidizi Utawala na Rasilimali Watu mkoa wa Mara Bi. Clothilde Komba akilezea umuhimu wa kikao cha Kamati ya Mkoa ya ulinzi wa Wanawake na Watoto kilichofanyika leo Mjini Musoma.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian Kitiku akielezea umuhimu wa jumbe katika kuleta hamasa kwa jamii katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichofanyika leo mjini Musoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara Bi. Neema Ibamba akieleza mikakti ya mkoa wa Mara katika kutekelza Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichowakutanisha kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto mkoa wa Mara.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mathias Haule akielezea umuhimu wa uwepo wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na Watoto kwa Kamati ya Mkoa wa Mara katika kikaokilichofanyika leo mjini Musoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na Watoto mkoa wa Mara wakifuatilia mada ,balimbali zizilokuwa zikitolewa katika kikao hicho kilichofanyika mkoani humo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Mwandishi Wetu Mara
Mkoa wa Mara umeweka Mipango dhatiti katika kuhakikisha wanapambana na vitendo vya kikatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kuhakikisha wanaifikia jamii katika kutoa ujumbe sahihi wa kuaondokana na vitendo vya kikatili hasa vitendo vya ukeketaji vilivyoshamiri mkoani humo.
Hayo yamebainika leo mkoani Mara wakati wa kikoa cha wadau kutoka Kamati ya Ulinzi ya Wanawake na Watoto pamoja na wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara kwa lengo la kupokea jumbe mbalimbali zitakazosaidia kuelimisha jamii ya mkoa huo kuondokana na mila potofu zinozopelekea vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto.
Akifungua kikao hicho Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bi. Vicky Mbunde amesema kuwa kwa Mkoa wa Mara kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 vitendo vya ukatili wa kijinsia vilikuwa asilimia 72 na vimepungua kufikia asilimia 66 mwaka 2015/2016.
Ameongeza kuwa tatizo la vitendo ya ukatili mkoa wa Mara sio vya kutengenzwa bali kwa kiasi kikubwa matatizo hayo husababishwa na mila potofu zinazochangiwa na uwepo wa mfumo dume ambayo inaathiri ustawi wa wanawake na watoto mkoani humo.
Bi. Vicky asema kuwa Serikali ya Mkoa wa Mara imejipanga katika kuhakikisha inatokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo utoaji wa elimu kwa kutumia jumbe zilizoandaliwa na mkoa kwa kutumia redio, magazeti na mikutano ili kuipa jamii uelewa wa juu ya madhara ya vitendo vya kikatili.
Ameutaja mkakati mwingine kuwa ni kampeni ya kila mwisho wa mwaka ambapo vitendo vya ukeketaji hufanyika ili kuihamasisha jamii kuachana na mila porofu zinazomgandamiza mwanamke na mtoto.
Akiwasilisha malengo ya kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa Clothilde Komba amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadiliana na kupata namana bora ya kupambana na vitendo vya ukatili mkoani humo.
Akiwasilisha jumbe katika kikao hicho Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian Kitiku amesema kuwa jumbe hizo muhimu sana katika kuhakikisha jamii inabadilika na kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Hivyo makala MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI
yaani makala yote MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mara-yapigilia-msumari-mapambano-dhidi.html
0 Response to "MARA YAPIGILIA MSUMARI MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI"
Post a Comment