Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake

Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake
kiungo : Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake

soma pia


Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri akizungumza na vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu vilivyopatiwa mikopo ya Serikali Dar es salaam Leo (PICHA NA HERI SHAABAN)


Na Heri Shaban
Mwambawahabari
MANISPAA ya Ilala Dar es salaam Leo wameanza rasmi kutoa mikopo ya Serikali kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu.

Zoezi la utoaji wa mikopo hiyo liliongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri ambapo kila kikundi kilipewa Hundi ya shilingi millioni 3 na Kikundi cha Vijana kilichopo Kitunda kilipewa milioni kumi.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es salaam Leo Jumanne Shauri aliagiza kila Kata Manisipaa Ilala waanzishe Viwanda vidogo vidogo ili waweze kukuza uchumi katika wilaya ya Ilala.

"Serikali yetu tukufu inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano John Magufuli Leo imetekeleza utoaji wa mikopo kwa awamu ya kwanza kwa  vikundi  mbalimbali ambapo Jumla ya shilingi 153,000,000 zimetolewa "alisema Shauri.

Shauri alisema dhumuni la utoaji wa mikopo hiyo wana Ilala wote hasa Wajasiriamali wawe maisha ya Kati waweze kujishughulisha  na Biashara na kujiingizia kipato chao.

Shauri aliwataka Wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala waliowezeshwa  fedha za Serikali watumie fursa hiyo katika kukuza mitaji yao  wakope warejeshe ili waweze kukopa tena.

Alisema Rais wa awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake alikuwa akipiga Vita maadui watatu Ujinga, Maradhi na umasikini,alitumia nafasi hiyo kuwataka Wajasiriamali hao wa Manispaa ya Ilala watumie mikopo hiyo kwa ajili ya kuzalisha Biashara wasitumie fedha hizo kwa ajili ya kuchangia harusi na ngoma.

Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mtaa na Watendaji wa Kata kusimamia vikundi vilivyopo katika kata za Manispaa ya Ilala.

Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa Ilala Fransisca Makoye alisema kigezo cha kwanza kwa mtu anayechukua mkopo lazima awe anatoka Manisipaa ya Ilala ajulike pia anatoka mtaa wake na kata malengo kufikia vikundi 1500 vya Manisipaa Ilala.

Aidha Makoye alitoa rai kwa vikundi vyote vilivyochukua mkopo kutumia fursa hiyo  katika kujiendeleza na kuweka Mikakati yao ya Biashara  na kujenga mtandao wao Wajasiriamali.

Alisema Halmashauri ya Ilala kama zilivyo Halmashauri nyingine imekuwa ikitekeleza kwa vitendo agizo LA Serikali linalotokana na azimio la BUNGE la mwezi Agosti 1993 .

"Agizo hili ilizitaka Halmashauri zote nchini kutenga na kupeleka asilimia 10 ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani Kwenye mfuko wa kuendeleza Wanawake na Vijana "alisema Makoye.

Alisema mpaka kufikia Mwaka 2018 Manisipaa ya Ilala imeshatoa kiasi cha shilingi 4,034,200,000 kwa wanufaika 15,388 kwa utaratibu wa awali.

Naye Mwenyekiti wa kikundi wa Betha Gruop cha Tabata Liwiti Salma Fumbwe alipongeza Serikali kufanikisha utoaji wa mikopo ya Wanawake.



Hivyo makala Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake

yaani makala yote Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/manisipaa-ya-ilala-yagawa-mikopo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Manisipaa ya Ilala yagawa mikopo ya Serikali kwa Wanawake"

Post a Comment