title : MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU
kiungo : MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU
MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAKAZI wa Kata ya Majohe kwa Ngosoma iliyopo Ukonga Gongo la mboto jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi kwenye kata hiyo ili kudhibiti matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara kiasi cha kusababisha hofu. Wakizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam jana na leo kwa nyakati tofauti wananchi wa kata hiyo wamesema matukio ya uhalifu yamekuwa yakitokea mara kwa mara , hivyo wanaamini kikijengwa kituo cha polisi itaisaidia kupunguza matukio ya uhalifu.
Wamesema Kata ya Majohe kwa Ngosoma inalo eneo kubwa na hivyo kuna idadi kubwa ya wakazi lakini cha kusikitisha hakuna kituo cha polisi licha ya jitihada mbalimbali kufanywa na Serikali za mitaa. "Kumekuwa na matukio ya uhalifu huku kwetu na sasa tumechoka kuendelea kushuhudia yakiendelea kutokea.
Tunaomba Serikali itusaidie kujenga kituo cha Polisi hasa kwa kuzingatia tayari eneo lilishatengwa na baadhi ya hatua za awali ziliasha. Tukiwa na kituo cha Polisi itasaidia kudhibiti uhalifu na wananchi tutakuwa na sehemu ya kukimbilia kutoa taarifa na kupata msaada wa Polisi,"amesema Shaban Said anayeishi mtaa wa Kichangani.
Ameongeza wiki mbili zilizopita saa mbili usiku , kuna watu wanaosadikiwa ni majambazi walivamia maduka yaliyopo eneo la Kona na kabla ya kupora fedha walijeruhi baadhi ya waliokuwamo kwenye maduka hayo na kisha kukimbia eneo la tukio hilo.
"Tukio ambalo nimelizungumzia ni moja tu lakini kuna matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea huku kwetu, hivyo kilio chetu wananchi wa Majohe Kwasoma tunaomba tujengewe kituo cha Polisi, tuko tayari kuchanga na nakumbuka kuna kikao kiliitishwa na wananchi wote tukakubaliana kuchanga fedha ili kituo cha Polisi kijengwe,"amesema Jumanne Joseph anayeishi Majohe Kona.
Kwa upande wa baadhi ya viongozi wa Kata ya Majohe kwangosoma wameiambia Michuzi Blog kuwa , kuna hatua mbalimbali ambazo znaendelea kuhakikisha kituo cha polisi kinajengwa hasa kwa kuzingatia eneo lipo na wananchi wanafahamu.
Hivyo makala MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU
yaani makala yote MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/majohe-kwangosoma-waiomba-serikali.html
0 Response to "MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU"
Post a Comment