MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI

MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI
kiungo : MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI

soma pia


MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI


Na. Mwandishi Wetu- MAELEZO

Mahakama ya Tanzania katika kusogeza huduma zake za utoaji haki kwa urahisi kwa wananchi, imelivalia njuga suala la uanzishwaji wa mahakama inayotembea yaani mobile court ili kusogeza huduma karibu zaidi na watanzania.

Akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari MAELEZO, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri katika Mahakama ya Tanzania Bi.Eva Kiaki Nkya amesema kuwa Serikali imeamua kuja na Mahakama zinazotembea ili kuwafikia wananchi kwa wepesi na kupunguza changamoto ya mlundikano wa mashauri katika Mahakama.

Alisema dhana ya Mahakama kuwafata wananchi siyo mpya kwani hapo awali kulikuwa na utaratibu huo ila kilichobadilika ni utaratibu wa kununua magari mawili ya awali ambayo ndani yatakuwa na mgawanyo wa chumba cha Hakimu pamoja na maafisa wa Mahakama.

Utaratibu huo mpya unatazamiwa kuanza katika Mikoa miwili ambayo ni Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Mkoa wa Mwanza kutokana na wingi wa mashauri , uchache wa Mahakama , pamoja na idadi kubwa ya wananchi.

“Serikali imeamua kuja na Mahakama zinazotembea ikiwa na lengo la kuwasogelea watu katika maeneo yao ili kuwapunguzia muda, kuwapunguzia gharama za wao kuifuata Mahakama badala ya wao kuifata Mahakama , Mahakama inawafuata wao”alisema.

Zamani tulikuwa tunatumia majengo ya Mahakama lakini sasahivi tumenunua magari maalum ambayo yataenda kusikiliza mashauri mtaani ili kurahisha huduma zetu.

Mahakama hizi zitakuwa na kazi ya kusikiliza mashauri ,kutoa elimu kwa umma na kufanya usuluhishi wa malalamiko ya wananchi, pia kutakuwa na utaratibu maalumu wa namna ya kusikiliza kesi na mpangilio wa kesi utategemea na tarehe tajwa. 

 


Hivyo makala MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI

yaani makala yote MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mahakama-inayotembea-mwarobaini-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI"

Post a Comment