KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU

KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU
kiungo : KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU

soma pia


KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha mmoja wa waasisi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ni pigo kubwa kwa Serikali kwani enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa kuhakikisha maono ya viongozi yanapata fursa ya kutekelezwa kwa vitendo.

Majaliwa amesema hayo leo Februari 27 , nyumbani kwa wazazi wake Ruge jijini Dar es Salaam wakati anatoa salamu za Serikali kutokana na kifo hicho ambapo amesema ni pigo kwa familia na zaidi ni pigo kwa Serikali. "Nimekuja hapa nyumbani kutoa salamu za pole kwa wazazi, familia, watoto, ndugu, jamii, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na Ruge Mutahaba.Kifo chake ni pigo kubwa kwa Serikali kwa nyakati tofauti tulikuwa tunashirikiana naye.Alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kuipenda nchi yao kwa vitendo.

"Ruge alitumia akili na aina ya maarifa yake kwa ajili ya kusaidia wengine, aliwahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii. Alisisimama imara kufanikisha falsafa za viongozi wakuu wa nchini kuanzia Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete na Rais wetu Dk.John Magufuli kuhakikisha vijana wanatumia fursa zilizopo nchini kufanya maendeleo. Tunaamini Ruge alikuwa ni kiongozi wa vijana wengine nchini,"amesema Waziri Mkuu.

Amefafanua kwamba wakati wote na kwa nyakati tofauti Watanzania walikuwa wakimuombea ili Ruge apate nafuu lakini ukweli leo hii hatunaye tena na kubwa zaidi ni kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele.

"Nirudie tena kifo cha Ruge ni pigo kubwa , alitumia fedha na mali zake kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania na amefanya mambo makubwa sana na ameshiriki kwa vitendo katika harakati za maendeleo ndani ya nchi yetu.Ruge amezunguka nchi nzima kupitia kampeni mbalimbali kuelezea umuhimu wa vijana kutambua nchi yao na kuwajengea uelewa wa kufanya mambo makubwa, "amesema Waziri Mkuu. 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi 'ubani wa msiba' Baba wa Marehemu Prof Mutahaba,alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi 'ubani wa msiba' Baba wa Marehemu Prof Mutahaba,alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia baadhi ya viongozi waliofika kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga ,alipokwenda alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 




Hivyo makala KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU

yaani makala yote KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/kifo-cha-ruge-mutahaba-ni-pigo-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU"

Post a Comment