title : KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN
kiungo : KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN
KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Kampuni ya Blockbonds yenye makao makuu yake nchini Norway kwa kushirikiana na Benki ya I & M ya Tanzania wamezindua rasmi huduma mpya bunifu ijulikanayo kwa jina la SPENN yenyekuweza kufanya malipo bure ya kutuma na kutoa hela.
Huduma hiyo bunifu itapatikana kupitia Benki ya I &M itakayokuwezesha kufanya miamala mbali mbali bure, ambapo utaweza kufungua akaunti binafsi na ya biashara kiganjani mwako.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds na SPENN Jens Glaso Jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa anafuraha kubwa kuingiza rasmi huduma hiyo katika soko lingine barani Afrika baada ya kufanikisha kuizindua rasmi nchini Rwanda mnamo Mwaka jana ambayo mpaka sasa inawatumiaji zaidi ya 130,000 nchini humo.
"Ni rahisi sana mtu yoyote anayemiliki simu aina ya Smartphone (simu janja) anaweza kujisajili na huduma ya SPENN Kwa urahisi ambapo ili kujisajili unapaswa kuwa na namba ya simu, jina kamili pamoja na namba ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na NIDA"amesema bwana Glaso.
Aidha mkurugenzi mtendaji Benki ya I&M Baseer Mohammed amesema kuwa benki hiyo imejikita zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ambayo huduma hiyo inalenga kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake.
"Huduma hiyo inayobadilisha namna ambavyo watanzania wanafanya miamala yao ya kifedha na kufanya mfumo mzima wa kufanya miamala kuwa na ufanisi zaidi, wenye usalama na pasipo kuwa na gharama, vilevile tunaamini kabisa huduma ya SPENN itachangia katika kuboresha maisha ya Watanzania "amesema Baseer Mohammed.
Hata hivyo Meneja masoko na mawasiliano Benki ya I & M Emmanuel Kiondo amesema kuwa sababu ya kutimia simu janja kupakua App ya SPENN na kufanya miamala yote iliyotajwa wamezingatia sababu za kiusalama zaidi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds na SPENN Jens Glaso akizungumza wakati wa uzinduzi huo kuhusu huduma hiyo ya SPENN inavyoweza kufanya kazi na kurahisisha kufanya kazi kwa kuondoa mfumo wa uchumi unaohitaji fedha taslimu kufanya miamala Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mtendaji Benki ya I&M Baseer Mohammed akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam kuwa Benki ya I &M imejikita zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ikiwa malengo yao ni kukidhi matarajio ya Wateja.
.Wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi huo wa huduma ya SPENN kwa kushirikiana na benki ya I & M Jijini Dar es Salaam
Hivyo makala KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN
yaani makala yote KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/kampuni-ya-blockbonds-kwa-kushirikiana.html
0 Response to "KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN"
Post a Comment