Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov

Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov
kiungo : Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov

soma pia


Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov

Pengine ulikuwa hujui jina BATE ni kifupisho cha Borisov Automobiles and Tractor Electronics, ndio! Nimetaja trekta, FC BATE inamilikiwa na kiwanda cha magari huko nchini Belarus. FC BATE wameshinda taji la Ubingwa wa ligi kuu ya Belarus mara 13 mfululizo, hawa ndio watawakaribisha Arsenal katika uwanja wa Borisov Arena Alhamisi hii majira ya saa 2:55 Usiku.

Mchezo wa Arsenal ni moja kati ya 16 itakayochezwa Usiku wa Alhamisi hii katika hatua ya 32 bora. Michezo ambayo kwa hapa Tanzania itarushwa na kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee kupitia chaneli zao za michezo.

Kwa upande wao Arsenal huenda wakaendelea kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Americk Aubameyang ambaye ni mgonjwa. Hata hivyo Arsenal watajipa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo baada ya kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya Huddersfield 2-1 katika ligi kuu ya Uingereza. Itakumbukwa pia msimu uliopita Arsenal waliichapa BATE 4-2 ugenini na kisha 6-0 katika dimba la Emirates, hivyo wataingia uwanjani historia ikiwabeba.

Kwa upande wa Chelsea wao watahitaji kuwa na utimamu wa kimchezo baada ya kufungwa ugenini kwa Manchester City kwa magoli 6-0 Jumapili iliyopita. Chelsea pia watakuwa ugenini nchini Sweden kucheza dhidi ya Malmo FF. Malmo imewahi kushinda mara moja tu dhidi ya timu za Uingereza. Mechi hii itaruka LIVE majira ya saa 5:00 Usiku kupitia ST World Football pekee.

Michezo mingine itayakayochezwa Alhamisi Usiku Saa 2:55 ni SS Lazio vs Sevilla (Sports Premium), Krasnodar vs Leverkusen (Sports Arena) na ile ya Saa 5:00 Usiku ni Sporting CP vs Villarreal (Sports Focus), Celtic FC vs Valencia CF (Sports Arena), FC Zurich vs Napoli SSC (Sports Premium) na nyingine zote kupitia chaneli za michezo sa StarTimes.

Michezo yote ya Europa league inaonekana kupitia StarTimes ambapo mteja anatakiwa kulipia kifurushi cha kati, kwa upande wa Antenna ni MAMBO Tsh 14,000 pekee na kwa upande wa dish ni SMART kwa Tsh 21,000 pekee. Pia mechi za Arsenal na Chelsea zina uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili.



Hivyo makala Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov

yaani makala yote Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/europa-league-arsenal-ugenini-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov"

Post a Comment