DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO

DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO
kiungo : DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO

soma pia


DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Rivets Resa Limited ya Mkoani Arusha Bahati Kittoh kulia akimkabidhi vifaa tiba Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto vyenye thamani ya milioni 400 kwa ajili ya kusambaza kwenye vituo mbalimbali vya Afya wilayani humo kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy katikati ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu 
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katika akiwa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DM) Flora Kessy kulia na Mkurugenzi wa Taasisi ya Rivets Resa Limited ya Mkoani Arusha Bahati Kittoh kushoto 
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba hivyo
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza ambapo pamoja na mambo mengine aliishukuru Taasisi hiyo kwa kusaidia vifaa tiba
Mkurugenzi wa halmashauri ya Muheza akizungumza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Rivets Resa Limited ya Mkoani Arusha Bahati Kittoh
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Rivets Resa Limited ya Mkoani Arusha Bahati Kittoh akizungumza kulia ni DMO wa wilaya ya Muheza Flora Kessy
wakiangalia mashine ya kufanyia mazoezi 
sehemu ya vifaa vilivyotolewa 


MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha vifaa vilivyotolewa na Taasisi ya Human Bridge ya nchini Sweeden vina sambazwa kwenye vituo vya afya kabla ya Machi 15 mwaka huu ili viweze kusaidia kutoa huduma. 

Agizo la Mkuu huyo wa wilaya alilitoa wakati akipokea vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya milioni 400 vilivyotolewa na Taasisi hiyo kupitia taasisi ya Rivets Resa Limited ya Mkoani Arusha kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha huduma za Afya kwenye maeneo yao. 

Alisema vifaa hivyo vipelekwe kwenye vituo vinavyotoa huduma kwa sasa na vile ambavyo havijakamilika havitapelekewa huko pindi vitakapokamilika huku akieleza kwenye maeneo ya changamoto ya umeme watasimamia kuhakikisha umeme unapatikana ili vifaa hivyo viweze kutumika kwenye matumizi yaliyokusudiwa. 

“Nikuagize Mkurugenzi wa Halamshauri hakikisheni vifaa hivi vinapelekwa kwenye vituo vya Afya vilivyopo wilayani hapa kabla ya Machi 15 mwaka huu kwa lengo la kuweza kusaidia kutoa huduma za Afya”Alisema DC huyo. 

Alisema haikuwa kazi rahisi kuweza kutengeneza orodha ya vifaa hivyo huko akipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kuwa karibu sana kuhakikisha vifaa hivyo vinafika wilayani humo 

“Lakini pia niseme kwamba hizo ni jitihada za serikali ya awamu ya tano kutokana na uchapakazi wake umekuwa chachu ya kuwavutia wadau mbalimbali wa maendeleo kuweza kuchangia na kuunga mkono harakati za wananchi kuweza kupata mafanikio kupitia sekta mbalimbali “Alisema 

“Tunawapongeza kwa kuguswa kwao kuona wasaidie kutoa vifaa tiba hivyo vya kutolea huduma kwa wilaya ya Muheza…vifaa vya sh.milioni 400 sio kitu kidogo tunawashukuru hatuna cha kuweza kuwalipa zaidi ya kuwaombea endeleeni kuisaidia wilaya ya Muheza ili iweze kuondokana na changamoto ya vifaa tiba”Alisema DC Mhandisi Mwanasha. 

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Flora Kessy alisema halmashauri hiyo iliomba vifaa tiba hivyo kwenye Taasisi ya Human Bridge ya nchini Sweeden yeye February 2 mwaka jana lengo likiwa kuweza kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vifaa tiba na vitandanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo. 

Alisema kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuboresha huduma za Afya na vitasambazwa kwenye vya kutolea huduma vitasambazwa kwenye kituo cha Afya cha Mkuzi ambapo watapeleka vifaa mbalimbali ikiwemo ultra sound,vitanda, magodoro, wheel chairs,vifaa vya upasuaji,vifaa vya macho na vifaa vya masikio . 

“Lakini pia halikadhalika vitapelekwa kwenye vituo vya Afya Ubwari ambazo ni kitanda cha chumba cha upasuaji,mashine ya usingizi,taa ya chumba cha upasuaji,mashine ya kusaidia upumuaji na ultrasound ikiwemo vituo vyengine vya afya kulingana na uhitaji kupitia taarifa za walezi wa zahanati husika”Alisema. 

“Kipekee niishukuru taasisi ya human bridge kupitia Taasisi ya Rivetsresa Limited iliyopo Arusha kwa kutupatia msaada wa vifaa tiba bila malipo yoyote…hakika hatuna cha kuwalipa lakini tutaendelea kuwaombea kwa Mungu pia tunahaidi kuendelea kuvitunza vifaa hivi”Alisema DMO huyo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bahati Kittoh wataendelea kuisapoti serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha changamoto ya vifaa tiba wanavitoa kila wakati vinapohitajika ili kuondokana na vikwazo ambavyo vilivyopo. 

“Kwanza nashukuru uongozi wote kuanzia DC pasipo yeye tusingeweza kujua mahitaji yenu DC aliweza kushughulikia mara moja ili kuweza kupatikana vifaa hivyo na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu..kwani tunaleta vifaa hivyo kwa sasabu vinahitaji sana kwa ajili kuwahudumia wananchi”Alisema. 

Aidha alisema wataendelea kuipa misaada ya namna hiyo wilaya hiyo ili kuhakikisha vikwazo vya vifaa tiba wanavyokumbana navyo wanashirikiana kuweza kuvitatua ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya. 

Hata hivyo aliwataka kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia kwani wao wanafanya kazi na serikali wataendelea kuisapoti serikali kwa vyotote itakavyokuwa ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana. 



Hivyo makala DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO

yaani makala yote DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/dc-muheza-atoa-maagizo-kwa-mkurugenzi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC MUHEZA ATOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO"

Post a Comment