title : VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU.
kiungo : VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU.
VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU.
Vijana wa Kanisa la Living Water Center Kawe chini ya Apostle Onesmo Ndegi na Apostle Lilian Ndegi lililopo katika Manispaa ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu katika kilele cha wiki ya vijana kanisani hapo.
Vijana hao waliamua kushiriki katika zoezi hilo mapema leo siku ya Jumapili ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi mpango wa Taifa wa Damu Salama chini ya Wizara ya Afya wa kutoa damu ili kuokoa uhai wa wahitaji wa damu katika hospitali nchini.
Akiongoza zoezi la uchangiaji damu Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo Albert Monyo aliwataka vijana katika jamii kuwa na moyo wa kutoa damu ili kuwasaidia wenye uhitaji maana kwa kufanya hivyo kunasaidia kupunguza uhitaji mkubwa wa damu uliopo kwenye hospitali nyingi hapa nchini.
Naye Afisa muhamasishaji Damu Salama kanda ya Mashariki Mariam Juma alitoa rai kwa waamini wa madhehebu mbalimbali na wanajamii kwa ujumla kujenga tabia ya kuwa wanachangia damu mara kwa mara bila kusubiri dharula.
Alisema uhitaji wa damu bado ni mkubwa na Ofisi ya Damu Salama bado hijawahi kuziba pengo la upatikanaji wa damu ya kutosha kwa asilimia mia moja.
Baadhi ya Vijana wachangiaji damu wakimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana kanisani hapo akimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo alipowaongoza vijana katika zoezi la uchangiaji damu
Afisa mshauri kutoka damu salama akimshauri mmoja wa wachangiaji damu katika zoezi hilo |
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara |
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara |
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo. |
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo |
Hivyo makala VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU.
yaani makala yote VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/vijana-watakiwa-kuwa-na-utamaduni-wa.html
0 Response to "VIJANA WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU."
Post a Comment