title : CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama
kiungo : CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama
CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Tabata Mtambani Heri Shaban (kulia) akikabidhi kanuni za Umoja wa Wanawake UWT Tawi la MTAMBAN Kwa Katibu wa UWT Mgeni Rumami (katikati) Mwenyekiti wa UWT Hamida Mstapha, hafla hiyo imefanyika Tabata Wilayani Ilala Dar es salaam Jana (PICHA NA CCM MTAMBAN)
Na Heri Shaban
CHAMA cha Mapinduzi CCM Tabata Mtambani kimesema kitawachukulia Hatua wanachama wa chama hicho watakaokichafua.
Tamko hilo limetolewa Dar es salaam Leo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Tawi hilo Hashimu Msekwa wakati wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani kuanzia Mwaka 2015/2018 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa mtaa huo Brigita Nchimbi.
Msekwa alisema tawi la Tabata Mtambani limejipanga vizuri katika kushika dola 2019 /2020 na kukiakikishia chama kinaibuka na ushindi mnono kila mwanachama atakayeomba kugombea atapewa nafasi hiyo mda ukifika wa uchaguzi wa Serikali za Mtaa, badala yake kwa sasa wachama wote wametakiwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa Mtaa aliyeopo madarakani
Alisema Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tabata Mtambani aliyepo sasa anatosha amewataka Wana CCM wote wampe Ushirikano Mwenyekiti huyo mpaka muda wake ukifika .
"Wana CCM wa Tabata Mtambani watakaobainika kuweka makundi na kukichafua chama hicho watachukuliwa hatua ikiwemo kupewa adhabu mpaka uchaguzi wa Serikali za Mtaa upite "alisema Msekwa.
Aliwataka wana CCM wote kujenga Umoja na kuakikisha wanachukua dola asubuhi.
Akisoma taarifa Nchimbi alisema katika kipindi cha 2018/2019 taarifa hiyo inaelezea mambo mbalimbali ya Maendeleo ambayo ametekeleza kwa kipindi hicho ikiwemo katika sekta ya elimu kwa muda 2015/2018 kiwango cha elimu kimepanda katika shule tatu zilizopo mtaa wa MTAMBAN Shule ya Tabata Jica, Tabata na Mtambani.
Nchimbi akielezea kwa upande wa sekta ya elimu alisema kwa Mwaka 2015 shule ya Mtambani wamefaulu 71 wasichana 37 Wavulana 34 ,Tabata 263 wavulana 137 wasichana 136 na Shule ya Msingi Tabata Jica 89 wasichana 51 wavulana 38.
Nchimbi alisema kwa Mwaka 2016 shule ya Msingi Mtambani waliofaulu 81 wasichana 42 wavulana 39 ,Tabata Wanafunzi 170 wasichana 81 wavulana 89 Jica 97 wavulana 50 Wasichana 47.
"Mwaka 2017 shule ya Msingi Mtambani waliofaulu 90 wasichana 25 wavulana 65 ,Tabata 183 wasichana 97 wavulana 86 Jica 133 wasichana 54 wavulana 59 na Mwaka 2018 Shule ya Tabata 206 wavulana 107wasichana 99 Mtambani 135 wasichana 81 wavulana 54 Jica 137 wasichana 76 na Wavulana 61"alisema Nchimbi.
Pia alisema katika kipindi cha uongozi wake Mtaa wa Tabata Mtambani wameunda vikundi 20 Kati ya hivyo vikundi 10 tayari vimesajiliwa vipo katika hatua ya kuchukua mikopo .
Aidha alisema amefanikisha ujenzi wa kisima cha maji kwa gharama ya shilingi milioni 19.9 fedha za Halmashauri ya Ilala kisima hicho kimekabidhiwa Serikali ya Mtaa bado kuzinduliwa..
Kwa upande wa Ulinzi Shirikishi Mtambani wamefanikiwa kwa asilimia 85 mtaa huo ipo amani ya kutosha kwa sasa, kuhusu Mazingira asilimia 95 Mazingira yapo masafi.
Nchimbi alisema kwa upande wa huduma za Jamii Wazee 30 wameshapewa huduma ya Bima ya afya Wazee 100 bado wanasubiria Halmashauri ya Manispaa ya wapigwe picha kwa ajili ya Bima ya Afya wale wa miaka 60 kwa sasa wamepewa Barua za Msamaha wa Matibabu kutoka Serikali ya Mtaa.
Hivyo makala CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama
yaani makala yote CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/ccm-tabata-mtambani-kuwachukulia-hatua.html
0 Response to "CCM Tabata Mtambani kuwachukulia hatua watakao kichafua chama"
Post a Comment