title : CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane
kiungo : CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane
CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane
Katibu wa CCM Kimanga Salma Kinyogoli akizungumza na wana CCM wa Kimanga Darajani katikra mkutano mkuu wa tawi (Kulia) Mwenyekiti wa CCM Kimanga darajani Ephraim Makoye (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mwenyekiti wa CCM Kimanga Tawi la Darajani akipokea taarifa katika mkutano mkuu wa tawi hilo Dar es salaam (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Heri Shaban
CHAMA cha Mapinduzi CCM Mtaa wa Kimanga darajani imewataka wana CCM wasichafune katika kipindi hichi cha kuelekea chaguzi za Serikali za Mtaa badala yake wanachama wa chama hicho wametakiwa wajenge chama na Jumuiya zake.
Hayo yalisemwa na Katibu Mwenezi wa CCM Kimanga Deogratus Mkude wakati wa hafla ya mkutano. Kuu wa CCM Kimanga darajani.
Mwenezi Deogratus alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi wa Serikali za mtaa kwa sasa sio mda wa kuchafuana ni mda wa kujenga chama pamoja na jumuiya za Vijana, Wazazi na jumuiya ya Wanawake UWT ili chama kiweze kushinda kwa kishindo.
"CCM kwa sasa ni mda wa kujipanga kuelekea chaguzi za Serikali za mtaa Natoa agizo sio mda wa kuchafuana katika mitandao na kujenga makundi ya uchaguzi kila mtu anatosha mda ukifika chama kitachagua"alisema Deogratus.
Deogratus alisema marufuku kwa mwana CCM yoyote kuchafuana kwani chama cha mapinduzi kinafundisha nidhamu Bora na kufuata misingi ya chama na kanuni.
Aliwataka wana CCM wote kuheshimu misingi ya chama cha mapinduzi na kufuata taratibu zake kujiandaa na chaguzi za Serikali za Mtaa.
Aidha pia aliwakumbusha wana CCM katika nyakati za kuelekea chaguzi za Serikali za Mtaa wanachama wa CCM wachague kiongozi Bora ambaye anakubalika na Wananchi ndani na nje ya chama.
Kwa Upende wake Katibu wa CCM Kata ya Tabata Kimanga Salima Kinyogoli aliwataka Wajumbe wa shina kila mmoja kutatua changamoto zake za mtaa na kuzifanyia kazi .
Salima alisema katika kero hizo zile ambazo zimekwama zipekekwe kata kwa ajili ya utatuzi kwani CCM ni chama kinachotekeleza ILANI ya chama.
.
Aliwataka viongozi wa chama kuongeza wanachama na kuwataka walipe ada ya chama kwa kila mmoja .
Wakati huohuo alisema 'Wagombea wenye nia ya kugombea uongozi wa chama lakini hawana sifa wasijisumbue kuchukua fomu ya uongozi majina yao yatakatwa.
Naye Mwenyekiti wa CCM Kimanga Darajani Ephirahim Makoye alisema Mtaa wa Kimanga Darajani una wakazi 12,892 wanachama wa ccm 374 kati yake wanaume 146 na Wanawake 228 akielezea hali ya uchumi kuna miradi minne ya chama.
Akielezea changamoto Makoye alisema Barabara kuu ya kimanga Kero, pamoja na barabara za ndani
Changamoto nyingine suala la ulinzi na Usalama changamoto pamoja na mikopo kwa Wanawake na Vijana, na wakandarasi wa takataka shida, ukosefu wa maji Salama ya bomba kwa Maneno na upanuzi wa mto Tenge.
Aliomba Serikali kutupia jicho changamoto hizo ili Kimanga iweze kuwa Kata ya mfano kwa Wilaya ya Ilala.
Mwisho
Mkutano wa CCM Kimanga ulifanyika January 30
Hivyo makala CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane
yaani makala yote CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/ccm-tabata-kimanga-yaomba-wanachama.html
0 Response to "CCM TABATA Kimanga yaomba wanachama wasichafuane"
Post a Comment