title : Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini
kiungo : Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini
Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini
Na Erick Msuya - MAELEZO
Wakati serikali ya Awamu ya Tano ikiwahangaikia wakulima nchini katika kuwawezesha kimaendeleo, wakululima na wadau wake wenye viwanda vya kilimo wameanza kuhamasishwa kufungua Bima ya wakulima itakayo wasaidia katika mazao yao.
Zaidi ya asilimia 70 ya watanzania nchini ni wakulima na ndio tegemeo kutokana na kilimo kuwa uti wa mgongo kwa taifa, hivyo kuwa na bima katika kilimo ni jambo ili kuzuia majanga katika mchakato wa kilimo kwa kuepuka moto, mafuriko, magonjwa ya mazao na mengine kadhaa.
Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) ni wadau wanao wanaosimamia shughuli za bima nchini na hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki katika sekta ya kilimo kwa wakulima kuwa na bima
Katika semina ya siku mbili februari 7 – 8, iliyofanyika jijini Dar es S alaam kwa lengo la kuwainua wakulima kwa kufungua bima za mazao ili kuwaokoa kiuchumi, wadau mbalimbali wa kilimo, sekta binafsi pamoja na serikali zimewataka wakulima kujiungta na bima ili iwasaidie pindi wanapokutana na majanga.
Akizungumza na Maelezo, Mkurugenzi wa Leseni na Mwenendo wa Soko kutoka Mamlaka ya Bima Tanzania, Samweli Mwiru amewataka wakulima nchini wajiandae kwa ujio huo wa bima katika mashamba yao pia watambue bima ni kitu muhimu hasa katika mazao yao na kilimo kwa ujumla..
“Bima itasaidia endapo patatokea majanga yoyote katika kilimo na mazao, makampuni ya bima nchini yataweza kuwalipa hizo gharama ili kumfanya mkulima kutofilisika na kumfanya aendelee na shughuli zake za kilimo” alisema Samweli Mwiru
Sambamba na hilo, amesema bima hiyo ya kilimo itamlinda mkulima katika maeneo mengi tofauti tofauti ikiwa na majanga yatokanayo na hali ya hewa, mjanga yatokanayo na Magonjwa mbalimbali ya Mimea, hivyo akaongezea kuwa bima hiyo itakuwa mahususi kukinga majanga yatokanayo na hali ya hewa.
Naye Afisa Habari wa Mamlaka hiyo, Eyuke Faustin amesema asilimia 68 ya wakulima wadogo wadogo elimu yao ni ndogo juu ya uelewa wa bima hivyo amewataka wadau mbalimbali wa bima hizo ingefaa waandae mchakato wa bidhaa za bei rahisi zitakazo weza kujibu maswali na changamoto zitakazo weza kumkabili mkulima.
“swala la bima kwa wakulima wadogo wadogo bado ni changamoto, kutokana na takwimu zilizopo zilizotolewa na Waziri wa kilimo, asilimia 68 ya wakulima wadogo wadogo elimu yao ni kuanzia elimu za msingi … kampuni za bima ziandae bidhaa rahisi zitakazo eleweka vizuri kwa kujibu hoja ama maswali ya mkulima mdogo mdogo” alisema, Eyuke Faustin.
Katika siku ya mwisho ya seminahiyo, matumaini yao ni kuandaa hatua za kuchukua katika kuendeleza soko la bima za kilimo, kuundwa kwa kikosi kazi maalumu kitakachoweza kuandaa ripoti itakayopelekwa wizarani ili mikakati itakayoandaliwa iweze kusaidia Mamlaka ya Bima pamoja na taasisi mbalimbali zilizo wadau.
Hivyo makala Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini
yaani makala yote Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/bima-ya-kilimo-kuwa-mkombozi-kwa.html
0 Response to "Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini"
Post a Comment