AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi

AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi
kiungo : AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi

soma pia


AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi


Na Philemon Solomon

BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imeendesha mafunzo maalumu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kwa shule za sekondari ili waweze kuzitofautisha taaluma hizo na ile ya wahandisi.

Akizungumza na wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi shule ya Azania Jijini Dar es Salaam February 21, 2019 Ofisa Mafunzo wa AQRB Matondo Daniel aliwataka wanafunzi kuutambua umhimu wa taaluma hizi katika mustakabli wa maendeleo ya taifa.

"Taaluma ya wataalamu wa Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi ni muhimu kwa taifa kutokana na uhaba wa wataalamu wa fani hiyo kwa sasa,"alisema Matondo na kuongeza kuwahamasisha wanafunzi wa sayansi kusoma taaluma hiyo ili kulipunguzia taifa changamoto ya wataalamu hao.
Alisema tathimini zinaonesha kuwa wataalamu wa fani hiyo ni wachache na kwamba mpaka sasa kuna Wabunifu Majengo 474 na Wakadiriaji Majenzi 427 nchi nzima hao ni wale ambao wanatambuliwa na Bodi.

Pia alisema kutokana na idadi hiyo ipo haja kwa taifa kuwa na idadi kubwa zaidi ili hapo baadaye taifa liwe na wataalamu wa kutosha katika taaluma hiyo ambao wataweza kusimamia nchi kuwa na makazi na majengo bora.

Akizungumzia upande wa sheria ya majengo alisema mpaka sasa bado haijawa tayari na kwamba serikali ipo mbioni kuikamilisha ili iweze kusimamia vyema majenzi na kuwabana wote ambao watakwenda kiyume cha taratibu kwa kuwapeleka kwenye vyombo husika ili sheria ifuate mkondo wake.

Kwa upande wao wanafunzi wa sayansi shuleni hapo wamefurahia sana kupata elimu juu ya utoafuti baina ya wahandisi na wajkadiriaji majenzi na kuiomba bodi kuendelea kuisambaza elimu hiyo kwa wanafunzi wengi zaidi ili aweze kuhamasika na kuzisomea taaluma hizo mara watakapomaliza masomo yao ya sekondari.

Godlove Kapufi mwanafunzi wa shule hiyo anayechukua PCM aliema kuwa anashukuru kupata elimu hiyo na atajitahidi kuwashawishi na wenzake kuisoma kwani anaamini iko katika soko.

"Sikuwa nafahamu kabisa taaluma hiyo, nashukuru sana AQRB kwa kutuelewesha naamini kufanya hivi kutatuwezesha kufanya uchaguzi mzri wa fani hapo mbele na kuweza kupunguza mzigo kwa serikali kwa kutokuwa na wataalamu wa kutosha wa taaluma hio,"alisema Kapufi.

Naye Mohamed Ally mwanafunzi mwingine wa kidato cha tano shuleni hapoa nayesoma PCM aliiomba bodi iishie hapo badala yake iendelee kuisambaza elimu hiyo nchi nzima ili vijana ambao ni wanafunzi wa sayansi waweze kuzitambua fursa zilizopo katika maomo hayo.

Alisema hapo awali wengi wao walikuwa wakijua mwanafunzi anayesoma sayansi anaweza kuwa daktari, mhandisi na zingine lakini walikuwa hawajui kama kuna taaluma ya wabuinifu majengo na wakairiaji majenzi.
 Ofisa Mafunzo kutoka Bodi  ya Usajili wa Wabunifu  Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Matondo Daniel akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya sekandari ya Azania jijini Dar es Salaam  juu ya umuhimu wa kusoma masomo ya  Sayansi.( PICHA NA PHILEMON SOLOMON).



Hivyo makala AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi

yaani makala yote AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/aqrb-yaendesha-mafunzo-maalumu-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi"

Post a Comment